Kwa mujibu wa wizara ya afya na Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma Jijini Dar es Salaam, Dkt. Mbarouk Seif Khaleif, ameeleza kuwa kila mwaka Watu 137,000 wanaugua Kifua Kikuu (TB) na wanaofariki ni 32,000 sawa na vifo 87 kila siku.
Aidha kati ya vifo, 33 ni vya waliokuwa wanaishi na Virusi Vya UKIMWI na kusababisha hasara inayogharimu kiasi cha 7% ya Pato la Taifa. Huku Mkoa wa Dar es Salaam ukiongoza kwa 17%.
Mgonjwa mmoja wa Kifua Kikuu ambaye hajagundulika na kuanza Matibabu anaweza kuambukiza Watu 10 hadi 15 kwa mwaka.
Leave a Reply