Wafikishwa mahakamani kwa madai ya wizi

Wafikishwa mahakamani kwa madai ya wizi

Wafanyakazi 4 wa kampuni ya JV SPEK LTD inayojenga mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga, Tanzania wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.

Watuhumiwa hao ni pamoja na waongoza mitambo Ally Said , Samwel Mtenga, Awadh Mrango na Zuberi Pastory Ally  ambaye ni dereva, wanadaiwa kutenda kosa hilo kwa siku tofauti kati ya Mei 01, 2023 na Juni 18 mwaka huu.

Aidha kwa mujibu wa mashtaka, thamani ya mafuta ni takribani Tsh. Milioni 20, watuhumiwa walikana mashtaka na kuachiwa kwa dhamana ya Milioni 5 kila mmoja kesi imeahirishwa hadi Julai 31mwaka huu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags