Wafariki kwa kula nyama ya kasa

Wafariki kwa kula nyama ya kasa

Watu saba kutoka kaya nne tofauti wamefariki baada ya kula nyama ya samaki aina ya kasa anayesadikiwa kuwa na sumu.

Kaimu RPC Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Canute Msacky amesema tukio hilo limetokea March 12  katika Kijiji cha Bweni na Kijiji cha Kanga, Wilaya ya Mafia.

Majina ya waliofariki katika tukio hilo ni Abdallah Hatibu Nyikombo 4, Makame Hatibu Nyikombo 9, Mohamedi Juma Makame Miezi 7, Ally Selemani Miezi 8, Salima Omary Mjohi 28, Minza Juma Hatibu Miezi 10 na Ramadhani Karimu Miezi 8.

Watu hao walifariki majira tofauti tofauti na miili yao imefanyiwa uchunguzi wa kitabibu katika Hospitali ya Wilaya Mafia na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.

“Chanzo cha tukio hilo bado kinaendelea kuchunguzwa, Watuhumiwa watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Wilaya Mafia kwa mahojiano zaidi, katika hatua hiyo Watuhumiwa hao wamelazwa katika Hospitalo ya Wilaya ya Mafia baada ya kuzidiwa wakiwa chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi, kwani nao walikula nyama ya samaki huyo”

Aidha Polisi inatoa wito kwa wavuvi Wilaya ya Mafia kuacha tabia ya kuvua samaki aina ya kasa ambao ni nyara za Serikali, bali wafuate taratibu na sheria za uvuvi wa samaki hao, Jeshi la Polisi litaendelea kuchukua hatua kali kwa Wavuvi wasiofuata taratibu na sheria za Nchi.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post