Wafanyakazi wa Ndege wanaswa wakiba vitu vya abiria

Wafanyakazi wa Ndege wanaswa wakiba vitu vya abiria

Wafanyikazi wawili wa Mamlaka ya Usalama wa Uchukuzi (TSA) wamefumwa wakiiba pesa na vitu vingine kutoka kwenye mifuko ya abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami Florida.

Kwa mujibu wa gazeti la New York Post inaeleza kuwa CCTV Camera zimenasa tukio la maafisa hao wawili wa usalama wanaodaiwa kuiba pesa kutoka kwenye mifuko, mabegi na vitu vyengine kutoka kwenye mizigo ya abiria kwenye kituo cha ukaguzi cha usalama.

Hata hivyo wafanyakazi hao wamekamatwa na wanakabiliwa na mashtaka ya wizi, ingawa maafisa hao kwa upande wao wamekana mashtaka hayo yanayowakabili licha ya kuoneshwa video ambazo ziliwaonesha wakifanya uhalifu huo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post