Wafanyabiashara wazuiwa kutoa mahindi nje ya nchi

Wafanyabiashara wazuiwa kutoa mahindi nje ya nchi

Wafanyabiashara wa mahindi kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wameegesha magari yao mpakani mwa Zambia wakishinikiza mamlaka nchini kuzungumza na serikali ya nchi hiyo ili iwapatie zaidi ya Tani 1,200 za mahindi wanazozishikilia.

Licha ya kununua kwa njia halali na kuwa na vibali vyote vya ununuzi na usafirishaji wa zao hilo, kwa zaidi ya miezi 5 mfulilizo mamlaka za Zambia zimeshikilia mizigo yao bila sababu maalumu.

Aidha, mkuu wa wilaya ya Momba, Fakii Lulandala, amesema tayari serikali ya Zambia imewataka wafanyabiashara hao kuuza mahindi hayo ndani ya nchi hiyo na si vinginevyo, huku akiwataka wafanyabiashara hao kuwa watulivu wakati suala hilo linatafutiwa ufumbuzi wa kudumu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post