WAAFRIKA WA KWANZA KUPANDA MLIMA EVEREST

WAAFRIKA WA KWANZA KUPANDA MLIMA EVEREST

Tukiwa tunaangazia watu ambao wamevunja rekodi mbalimbali barani Afrika, LISTI inaletea wakali wa kwanza kabisa kuwahi kuvunja rekodi ya kupanda mlimi mrefu zaidi duniani, MLIMA EVEREST.

 

  1. SIBUSISO VILANE

Kati ya milima mirefu duniani, Mlima Everest, ambayo ni sehemu ya safu ya milima ya Himalaya, katika bara la Asia, ndio mlima unaoongoza kwa urefu duniani, ukiwa na urefu wa mita 8,848 juu ya usawa wa bahari.

Sibusiso Vilane, mwenye raia ya Afrika Kusini alivunja rekodi hii mwaka 2003 na  kuwa muafrika wa kwanza duniani kupanda mlima huo hadi kufika kileleni. 

Alianza safari yake mwezi Machi 2003, na kumaliza mwezi Mei 2003.

 

  1. SARAY KHUMALO

Rekodi hiyo ya kupanda mlima Everest inakuja kuwekwa pia na mwanadada Saray Khumalo, kutoka hukohuko Afrika Kusini, ambae yeye anakuvunja rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kuupanda mlima huo hadi kileleni.

Saray Khumalo alipanda mlima huo mnamo mwezi Mei, mwaka 2019, ikiwa ni mara yake ya 3 kujaribu kupanda mlima huo, huku mara zingine mbili, alishindwa kupanda kwa sababu mbalimbali, ikiwemo tetemeko la ardhi, iliyoikumba Nepal, mwaka 2015.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags