Vyombo vya habari kuchunguzwa

Vyombo vya habari kuchunguzwa

Waangalizi wa vyombo vya utangazaji vya nchini Uturuki, jana Jumanne, wametangaza kuchunguza vituo sita vya televisheni vya upinzani kwa madai ya kukashifu umma kupitia matangazo ya duru ya pili ya uchaguzi wa Rais siku ya Jumapili.

Mmoja kituo kimoja kinacho chunguzwa, kimesema kupitia tovuti yake kwamba hatua hiyo inaonyesha namna serikali inavyobana kituo hicho na kazi zake.

Madai hayo yametokea siku mbili baada ya Rais Tayyip Erdogan wa chama cha haki na maendeleo (AKP) kutangazwa mshindi wa uchaguzi baada ya kufanyika duru ya pili ya uchaguzi wa rais Jumapili.

Kamati ya kulinda wanahabari imedai kwamba ukiukwaji wa uhuru wa vyombo vya habari ulifanyika na kabla uchaguzi wanahabari kadhaa walikamatwa, kushikiliwa jela na kudhalilishwa kwa kuripoti uchaguzi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags