Vita ya Diamond na Alikiba imevuka mipaka

Vita ya Diamond na Alikiba imevuka mipaka

Baada ya nyota wa muziki #Diamondplatnumz, kutupa dongo upande wa pili mara tu wimbo mpya wa #Zuchu kufanya vizuri na kuingia trending number one kwenye mtandao wa #YouTube, vita imeendelea kuwa kali kwenye mitandao ya kijamii kati ya msanii #Alikiba na #Diamond.

 Ushindani wa wasanii hawa unaonekana  kuvuka mipaka kwani msanii #Alikiba ameshindwa kukaa kimya na kujibu mashambulizi kwa #Simba huku Diamond nae akiendelea kurusha madongo na kufikia kutaja jina la mke wa #Alikiba, jambo ambalo limewaweka wengi kwenye viulizo, huku akidai kuwa licha ya kumkuta #King kwenye muziki lakini bado amempita kwenye kila kitu.

Diamond kupitia #InstaStory yake ambayo anatumia kurusha madongo hayo anadai kuwa yeye ndiyo sababu ya hadi leo #King anaendelea kusikika, na anadai kuwa Mfame hana roho ya kusaidia ndiyo maana ameshindwa kumsaidia hata mdogo wake kufanya vizuri kwenye muziki.

Kelele zote hizo zimeibuka baada ya #King kumjibu #Mond kupitia ukurasa wake wa #Twitter kwa kudai kuwa #Diamond anawekeza pesa kwa ajili ya kuwafanyia figisu wasanii wengine huku akimtaka aache wivu.

Unadhani vita hii inajenga au inabomoa?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags