Visa vya Aunty Ezekiel na Ruby juu ya Kusah

Visa vya Aunty Ezekiel na Ruby juu ya Kusah

Bwana bwana! Wanaanza kumchokoza Ruby wetu.

Kama tunavyojua bwana... msanii wa Bongo Fleva, Kusah amewaweka katika kipindi kikali wasanii Aunty Ezekiel na Ruby, kwa sasa maarudy kama "Zena na Betina" kwa vijembe na vituko wanavyorushiana mitandaoni.

Ikumbukwe kuwa kwa sasa Aunty Ezekiel ameolewa na Kusah, na wawili hao wamefanikiwa kuwa na mtoto mmoja wa kiume.

Matashitit hayo yalianza baada ya Kusah kuachana na Ruby (ambae wamezaa nae mtoto mmoja pia), huku Ruby akishtumu kuwa Kusah hahudumii wala kumuona mtoto, na mambo mengine mengi kama vile Kusha ni mchawi na kadhalika.

Vita yote hii, inasemekana ni wivu tu wa Ruby juu ya Aunty, ingawa Ruby mwenyewe amekanusha, akisema "kwa kipi???"

Hata hivyo, juzi kati Kusah aliuliza fans wake wamuambie wanatamani atoe nyimbo na nani, na mkewe Aunty Ezekiel akamtaja Ruby.



Zena acha kumchokonoa betina jamanyy, msimuamshe Ruby alielala, hayaa...

Tuambie uko upande gani?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags