Viongozi wa kijiji wajiuzulu kisa umeme

Viongozi wa kijiji wajiuzulu kisa umeme

Kutokana na serikali kushindwa kupeleka nishati ya umeme katika kijiji cha Uhambule wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe Wenyekiti wa vitongoji 3 pamoja na wajumbe 7 wa Serikali wamejiuzulu.

Kwa madai ya kuwa serikali imeshindwa kupeleka nishati ya Umeme kwenye maeneo yao licha ya kuahidiwa kwa muda mrefu.

Mkuu wa wilaya hiyo Claudia Kitta amewataka viongozi hao kurejea kwenye majukumu yao kwa kuwa serikali inaendelea kutoa huduma hiyo na imekusudia kufikisha umeme kwenye kila kitongoji.

“Hili linatusikitisha lakini mpango wa Serikali ulianza kwa awamu na upande wa vitongoji tayari serikali imeanza kutekeleza”alisema mwenyekiti huyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post