Kundi la viongozi wa kanisa la kianglikana kutoka sehemu mbalimbali duniani wamemkataa Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby, kuwa kiongozi wao baada ya Kanisa la Uingereza kuunga mkono maombi ya baraka kwa wapenzi wa jinsia moja.
Maaskofu wakuu wanaowakilisha majimbo 10 kati ya 42 katika Ushirika wa Kianglikana wametia saini taarifa wakisema hawamfikirii tena Welby kama kiongozi wa usharika wa kimataifa.
Ni mara ya kwanza kwa uongozi wa Askofu Mkuu wa Canterbury kukataliwa na kundi kubwa la makanisa.
Leave a Reply