Vihatarishi vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Vihatarishi vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Magonjwa  yasiyo ya kuambukiza huchangia katika kumi bora ya vifo duniani katika nchi zenye uchumi mdogo, wa kati na wa juu, takwimu zilizotolewa na shirika la afya duniani, WHO. Mifano ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni pamoja na; kiharusi, ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa akili na kansa. Utafiti wa kiafya unaonesha mitindo hatarishi ya kimaisha hupelekea ongezeko la hatari ya kupata  magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

 

MAMBO HATARISHI YANAYOPELEKEA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA.

Magonjwa yasiyo ya kuambukiza muda mwingi hayasababishwi na vijidudu vinavyosambaa kutoka Kwa mtu mmoja hadi mwingine Ila ni mtindo wa maisha wa binadamu unaoleta hatari ya kupata magonjwa haya. Mambo hayo hatarishi ni pamoja na;

Sukari ya damu ya kufunga.

Kiwango kikubwa cha sukari ya damu ya kufunga huashiria kisukari au upinzani wa insulini. Kiwango kisicho cha kawaida cha chini cha sukari ya damu ya kufunga husababishwa na dawa za kisukari.

Mwili unahitaji glukosi ili kupata nguvu na glukosi hupatikana katika chakula mtu anachokula, ingawa sio glukosi yote inatumika mara moja. Insulini hufanya uwezekano wa kutunza na kuachia glukosi. Baada ya mlo, kiwango cha sukari kwenye damu huongezeka na hufikia kilele saa moja baada ya kula.

Sukari ya damu ya kufunga hutegemea mambo matatu; yaliyomo kwenye mlo uliopita, ukubwa wa mlo uliopita na uwezo wa mwili kuzalisha na na kujibu insulini.

Kiwango cha sukari kwenye damu katikati ya milo inaonesha namna gani mwili inasimamia sukari, kiwango cha sukari kubwa ya kufunga inapendekeza kuwa mwili haukuweza kushusha kiwango cha sukari kwenye damu. Hii hupelekea upinzani wa insulini, uzalishaji hafifu wa insulini na muda mwingine vyote kwa pamoja.

Shinikizo kubwa la damu.

Shinikizo kubwa la damu kimya kimya huweza kuleta madhara kwenye mwili kwa miaka mingi kabla ya dalili kujitokeza. Shinikizo la damu lisipodhibitiwa hupelekea ulemavu, maisha ya kiafya duni, mshtuko hatari wa moyo na hata kiharusi. Matibabu na kubadili mtindo wa kimaisha husaidia kudhibiti shinikizo kubwa la damu kupunguza hatari ya matatizo ambayo ni tishio kwa maisha ya mwanadamu. Shinikizo kubwa  la damu hupelekea ateri kuharibiwa na kupungua, ugonjwa wa moyo, moyo na figo kushindwa kufanya kazi,  upofu, upotevu wa kumbukumbu, ugonjwa wa akili, nevu kuharibika na kiharusi.

 

Kolesteroli

Baada ya muda fulani kiwango cha kolesteroli kikiinuliwa huharibu ateri, hupelekea ugonjwa wa moyo na kupata hatari ya kiharusi. Ikibidi punguza kiwango kikubwa cha kolesteroli kwenye mlo, fanya mazoezi na tumia dawa. Mazoezi pekee huongeza kiwango kizuri cha kolesteroli lakini hayapunguzi kiwango kibaya cha kolesteroli. Kolesteroli nyingi haina dalili, hivo kolesteroli katika damu inabidi kuangaliwa mara kwa mara. Kula vyakula vya mafuta sana na pombe nyingi husababisha ini kuzalisha kolesteroli nyingi kwenye damu. Njia zisizo za kitabibu za kupunguza kolesteroli ni kama, kuacha kuvuta sigara, kupunguza pombe na kudumisha uzito wa mwili kiafya.

  

Matumizi hatarishi ya pombe.

Magonjwa sugu hutokea Kwa watumiaji wa pombe nyingi katika kipindi cha miaka kadhaa, matumizi ya pombe huchagizwa na hatari ya kupata matatizo ya kiafya kama majeraha yatokanazo na ajali za barabarani, matatizo ya akili, msongo wa mawazo na upotevu wa kumbukumbu. Unywaji wa pombe kupita kiasi hushambulia kinga ya mwili na Kupunguza seli za kinga na kuongeza nafasi kubwa ya kushambuliwa na maradhi kama pneumonia, kifua kikuu, UKIMWI n.k pia unywaji wa pombe nyingi husababisha kutanuka Kwa misuli ya moyo, mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida, kiharusi na shinikizo kubwa la damu. Poa huleta madhara kwenye ini.

Kutokufanya mazoezi.

Kutokufanya mazoezi mara Kwa mara inayoambatana na Lishe mbovu hupelekea magonjwa ya moyo yanayoambatana na unene, shinikizo kubwa la damu, kiharusi, kisukari, kiwango kikubwa cha kolesteroli ambayo ni tishio Kwa afya ya binadamu.

Unene

Watu wenye unene na uzito kupita kiasi wako kwenye hatari ya kupata matatizo ya shinikizo kubwa la damu, kiwango kikubwa cha kolesteroli, kisukari, tatizo kwenye mifupa na jointi, kukosa usingizi na matatizo ya kupumua, maisha duni ya kiafya, matatizo ya kiakili mfano msongo wa mawazo na maumivu ya mwili na mwili kushindwa kufanya kazi vizuri.

Uvutaji wa sigara

Unapovuta sigara kemikali hatari huingia katika mapafu na kusambaa katika mwili. Zinaweza kufikia moyo na ubongo sekunde kumi tu baada ya kuvuta pafu lako la kwanza na kwenda kila mahali damu inapofika na kuathiri kila sehemu ya mwili. Uvutaji wa sigara husababisha kansa za aina mbalimbali, kansa ya mapafu, ini, kibofu, koo, figo na damu. Pia hupelekea matatizo ya upumuaji, magonjwa ya moyo, kiharusi na huathiri mzunguko wa damu na pia huleta utasa.

 

UDHIBITI WA TABIA HATARISHI ZINAZOPELEKEA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA.

Moja ya njia muhimu sana ya kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni kudhibiti vyanzo hatarishi vinavopelekea mlipuko wa magonjwa haya. Njia hizi ni kama;

  • Kupunguza matumizi ya sigara na matumizi mabaya ya pombe
  • Kula lishe bora iliyokamilika.
  • Kufanya mazoezi mara Kwa mara.
  • Kuwa na mtindo mzuri wa kimaisha
  • Kwenda kwenye vituo vya afya kupima na kupata tiba.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags