Video za ukatili zafanya Lebron afute urafiki na Diddy

Video za ukatili zafanya Lebron afute urafiki na Diddy


Mcheza mpira wa kikapu wa NBA Lebron James amefuta urafiki na Diddy kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya video za hizi karibuni kusambaa zikimuonyesha msanii huyo akimpiga aliyewahi kuwa mpenzi wake Cassie kwenye ukumbi wa Hoteli.

Ikumbuke kuwa baada ya kuandamwa na kesi za unyanyasaji wa kingono toka mwishoni mwa mwaka jana mkali huyo wa muziki wa hip-hop kutoka Marekani jana Jumamosi, 18 Mei, 2024, zilisambaa video kupitia mitandao ya kijamii zikimuonyesha akimpiga na kumtolea maneno aliyekuwa Cassie.

Video hiyo kwa mara ya kwanza ilioneshwa kwenye runinga ya Cnn Diddy akionekana akimpiga Cassie ngumi usoni na kumburuza kwa hasira kwenye hotel ambayo walikuwa pamoja iliyopo jijini Los Angeles nchini humo.

Aidha kwa mujibu wa runinga hiyo ilieleza kuwa tukio hilo lilitokea mwaka 2016 huku ikidaiwa Diddy alitoa zaidi ya milioni 100, kwa hoteli hiyo ili kuzuia video isitoke.

Diddy amekuwa akiandamwa na kesi za unyanyasaji wa kingono tangu Desemba 2023 ambapo mpaka kufikia sasa wanasheria wake wanaendelea kupambana mahakamani na kesi hizo.

Hata hivyo, baada ya kusambaa Mwanasheria wa Wilaya ya Las Angeles, DA George Gascón aliweka wazi kuwa Diddy hawezi kushitakiwa kwa video hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya mwanasheria huyo sababu kuu inayomfanya asishitakiwe ni kuwa tukio limeshapita muda wake.

Hata hivyo, taarifa hiyo ilidai kuwa ni ngumu kufananisha tabia ya mtu aliyokuwa nayo mwaka 2016 na sasa na endapo tabia hiyo ingetokea mara nyingi basi Diddy angeweza kushitakiwa.

“Kufikia leo, watekelezaji wa sheria hawajawasilisha kesi inayohusiana na shambulio lililoonyeshwa kwenye video dhidi ya Bw. Combs, lakini tunahimiza mtu yeyote ambaye amefanyiwa ukatili au ana ushahidi wa hivi karibuni atoe taarifa kwa vyombo vya sheria au kuwasiliana na ofisi yetu ya Huduma za Waathiriwa,” DA George Gascón alisema.

Sheria ya California kwa wahanga wa shambulio lolote wanatakiwa kufungua mashitaka muda wa shambulio au mwaka mmoja baada ya tukio, hivyo kulingana na ratiba ya tukio, hakuna mashitaka yanayoweza kumfanya Diddy akamatwe.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags