Video ya tiktok yafanya admin wa Napoli aache  kazi

Video ya tiktok yafanya admin wa Napoli aache kazi

Msimamizi wa mitandao ya kijamii ya ‘klabu’ ya #Napoli Alessio Fortino ameamua kuacha kazi baada ya mchezaji wa ‘timu’ hiyo Victor Osimhen kudhihakiwa kutokana na video mbili ‘zilizopostiwa’ na ‘klabu’ hiyo katika mtandao wa TikTok.

Aidha kutokana na video hiyo mshambuliaji huyo alichekwa na kusemwa vibaya kwa kukosa ‘penati’ dhidi ya Bologna kabla na kuitwa ”Nazi” jina ambalo limechukuliwa kuwa la kibaguzi.

Baada ya video hizo kusambaa, wakala wa Osimhen alijibu na kusema kitendo hiko hakikubaliki na kutaka kuishtaki ‘klabu’ hiyo.

Kupitia mtandao wa #Instagram Fortino ametangaza uamuzi huo kwa kuandika “baada ya siku 805 safari yangu kikazi na Napoli inafikia mwisho”.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags