Video ya Diddy akimpiga Cassie yavuja

Video ya Diddy akimpiga Cassie yavuja

Baada ya kuandamwa na kesi toka mwishoni mwa mwaka jana Mkali wa Hip-hop kutoka Marekani huenda akafunguliwa mashitaka kutokana na video inayoendelea kusambaa kupitia mitandao ya kijamii akimpiga aliyekuwa mpenzi wake Cassie.


Video hiyo ambayo imeoneshwa kwa mara ya kwanza kwenye runinga ya Cnn imemuonesha Diddy akimpiga Cassie kwenye hotel ambayo walikuwa pamoja iliyopo jijini Los Angeles nchini humo.


Aidha kwa mujibu wa runinga hiyo tukio hilo lilitokea mwaka 2016 huku ikidaiwa kuwa Diddy alitoa zaidi ya milioni 100 kwa hoteli hiyo ili kuzuia isitoke.


Diddy amekuwa akiandamwa na kesi za unyanyasaji wa kingono tangu Desemba 2023 ambapo mpaka kufikia sasa wanasheria wake wanaendelea kupambana Mahakamani na kesi hizo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags