Vazi linalo badilika muundo ndani ya sekunde
‘Kampuni’ ya Software Adobe kutoka nchini Marekani nimewashangaza wengi baada ya kuzindua nguo aina ya gauni ambalo linaweza kukubadilisha muonekano kila utakapo hitaji.
Vazi hilo la teknolojia limepewa jina la Project Primrose, ambalo unatumia kitufe kubofya na kubadilisha muundo na muonekano ndani ya sekunde.
Christine Dierk aliongoza onesho hilo Oktoba 10, jijini Los Angeles huku ikielezwa kuwa vazi hilo linaweza hata kutambua mwendo wa mvaaji, na kufanya muundo kuyumbayumba na kulegeza mwelekeo anapoenda mvaaji.
Leave a Reply