Vazi la kanzu lilivyo tamba sikukuu ya eid

Vazi la kanzu lilivyo tamba sikukuu ya eid

Mambo niajeeee!!! Najua mko poa sana watu wangu wa nguvu leo sasa katika mambo yetu yale ya fashion tunaendelea kukujuza mambo kadha wa kadha yanayo usiana na urembo, kupendeza na fashion kwa ujumla sijui umenipata hapo mwanetu haya sasa tendelee.

Kumbuka msimu wa sikuku ndio hii week sasa lazima twende na fashion bhana kama ulikuwa una jiuliza utatokaje yaani mambo ya kutupia viwalo usiwaze sisi watu wa fashion tutakusaidia lakini kama utapenda.

Week iliopita tulikuwa upande wa wanawake na vazi lao la abaya linavyo trend kuelekea sikukuu ya Eid, na tulipata koment nyingi sana kuhusiana na watu walivyoipokea.

Leo bhana tunahamia upande wa wanaume na hatuja waacha nyuma jamani katika vazi la kanzu kuelekea sikukuu ya Eid ungana nasisi kujua mengi zaidi kuhusu vazi la kanzu.

Vazi la kanzu ni vazi la dini ambalo huvaliwa na wanaume ni vazi la rangi nyeupe au nyengine ambazo tangu kale huvaliwa muda mwengine vazi hili linaingiliwa na wanawake katika maeneo mengi kama vile bonde la mto indus, Nigeria na nchi za uarabuni huko.

Lakini siku hizi matumizi yake yamepungua katika ustaarabu wa watu wa magharibi sana sana  imebaki katika dini hasa dini ya kiislamu wanaume huvaa kanzu wanapo ingia msikitini au muda mwengine kwenye miadhara yao muda mwengine wanavaa mahali popote.

Pia hivi karibuni vazi hilo limekuwa kama fashion tu kama ilivyo kwa upande wa wanawake na vazi la abaya, kwa upande mwengine wanaweke nao wamekuwa wakiliingilia vazi hilo.

Kuongeza chachu kwa wafanya biashara wengi kuuza kanzu mpaka mtu unashindwa uwende wapi sasa kina chofata mtu kulinganisha bei ya duka moja la kanzu na duka jengine mara nyingi wakiona unafuu upo wapi ndipo watakapoenda kununua kwa hapa Tanzania.

Lakini vazi la kanzu ni aghalabu kushonwa kwa hapa Tanzania so mara nyingi vazi hilo wafanyabishara ufuata linapopatikana nchi za watu kama vile dubai, omani,uturuki na kwengineko.

Haya sasa sisi hatukuwa nyuma basi tukaamua kukusogezea wafanya biashara ili kuweka wazi nini wanapitia katika bishara hiyo gharama zao, changamoto wanazo kumbana nazo na niwapi sana sana wanapo kwenda kuchukua bidhaa hizo za kanzu, kwa kindipi hiki cha sikukuu ya Eid kama tunavyojua kunakuwa na uhitaji mwingi.

Tulipata wasaa wakuzungumza na Omary Omary mfanyabiashara wa vazi la kanzu kutokea Sinza Dar es salaam imezoeleka kuwa vazi hilo halina hamasa kubwa kwa hapa Dar es salaam bara mpaka uwende visiwani Zanzibar.

Kwa upande wa kijana Omary yeye anatukanushia kauli hiyo bana anasema sikuhizi mambo yamebadilika kila pahali watu wanauza kanzu tena kwa bei tofauti kulingana na mfanyabiashara mwenyewe anavyo taka.

Kwasababu uhitaji wavazi hilo katika jamii umekuwa mkubwa sana hali ambao inasababisha soko kupanuka kwa kiasi kikubwa

Hatu kukwamia hapo tuliendelea kumuuliza biashara yake huwa anaifanya kwa mtindo gani ili wateja wa mfike ilipokuwa biashara yake anaeleza kuwa

“Kama ilivyozoeleka saivi biashara bila kupitia mitandao ya kijamii inakuwa bado ujawafikia wateja na inakuwa ngumu kwa hiyo mimi nafanya kama wafanyabiasha wenzangu naitangaza biashara yangu kupitia mitandao ya kijamii watu wanaona wakivutiwa wanakuja lilipo duka langu au wengine wanafanya deliver basi mtu anaupata mzigo wake hapo alipo” amesema Omary

Aidha  tulizungumza nae kuhusu bei zake yeye zipoje na kutudadavulia kuwa “Unajua vitu hivi niadimu hapa kwetu kwa hiyo lazima viwe na thamani kidogo mimi kanzu huwa nauza kuanzia elfu 65 mpaka laki na 60 na nina wanogeshea wateja wangu kwa kuambatanisha kanzu, kobazi, kofia au kiremba na saa hiyo inakuwa full parckage inanogesha wateja na inakuwa rahisi kuwapata” alisema Omary.

Mbali na hayo kijana huyo pia alitueleza kuwa bidhaa zake yeye huwa anazifata kutoka Oman kupitia wafanyabiashara wa huko huko kama wengi wao wanavyo fanya.

Tunajua siku zote hakuna kitu kisicho kuwa na changamoto yeye alifunguka kwa kusema

“Changamoto inayo niumiza kichwa pale tunapofika nchini ukaguzi unakuwa mkubwa sana kiasi kwamba itatafutwa sababu ili mradi ulipe faini kingine waweza ukabadilishiwa mzigo ukifika huku unapata hasara kwasababu mteja alie agiza lazima atakataa kanzu kwasababu sio alio itaka hapo lazima uuze bei ya hasara ili mradi umalize mzigo” amesema Omary

Hatukuridhika na bwana Omary safari ikaanza tukatua mpaka Magomeni Mapipa tukakutana na mfanyabiashara mwengine aliejulikana kwajina Maher Abdulkareem kwa upande wake yeye ameeleza biashara yake wateja wamekuwa wakimiminika kama mvua

Hasa kuelekea msimu huu wa sikukuu ya Eid japo bei ya kanzu hupanda na kushuka lakini imekuwa haiboi kwa sababu yeye bidhaa zake ni brand kubwa. Kwasababu najulikana sana kupitia mitandao ya kijamii haswa haswa Tiktok.

Yeye pia hufuata nguo hizo nchi za nje japo yeye huwa anaenda sehemu tofauti tofauti kama Dubai na Oman mwamba anatueleza kuwa

 “Mimi huwa naendana na wateja wangu wana uwezo wakumiliki kanzu za ya aina gani kwani material ya kanzu yana kuwa tofauti sasa mteja akija hapa tuna mfafanulia kama kanzu ya eflu 40 haiwezi kuwa sawa na material ya kanzu ya elfu 60 so swezi kumficha mteja niyeye aamue kuchukua kanzu ya bei gani” amesema Maher

Kwa wasiomjua Maher bwana ni kijana ambae anatrend sana kupitia mtandao wake wa kijamii wa Tiktok kutokana na biashara yake anayoifanya ya kuuza kanzu.

Nyie nyie!!nasema vipi usiache mambo yakupite kama upepo bhana fanya kweli basi kijana hilo vazi lisikukose uende na fashion upate kanzu ya kuswalia Eid bhana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post