Hello mambo vipi!! Leo katika ulimwengu wetu wa fashion kama kawaida tunaendelea kukusogezea mambo mbalimbali yanayo husiana na urembo, mitindo, na fashion kwa ujumla.
Kama tunavyojua binti mrembo lazima uwe unabadilika madilika na mitindo kama dunia ya sasa inavyo hitaji, mfano huu ni mwezi wa ramadhani kwahiyo inabidi uendane na mwezi huu kimavazi, tabia namuonekano.
Ukiachilia mbali mwezi huu pia kuna sikuku idi ambayo hufanyika baada ya kumaliza mfungo wa ramadhani, so watu wanakuwa wanavaa sana vazi hilo, tumetafuta wauzaji na kuzungumza nao kuhusiana na biashara msimu huu na unaokuja hivi karibuni. Ungana nasi mwanzo mpaka mwisho uweze kujua.
Leo bwana tumekusogezea vazi la Abaya, je unajua kuwa abaya ni nini, najua kabisa unatamani mno kujua kuhusiana na vazi hili, maana limekuwa linatrendi sana kwenye status, japo neon hili la ‘abaya’ wengi limewachanganya kidogo ila ungana nasi mwanzo mpaka mwisho kujua kuhusiana na vazi hili.
Abaya nivazi jeusi au rangi yoyote ya kung’aa linalo valiwa juu ya nguo kama pazia la mwili, ni vazi la wanawake hususani wa Kiarabu, waswahili kama sie huliita vazi hilo baibui ni vazi linalo kuonyesha mwenye heshima na huvaliwa haswa na watu wa zehebu la kiislam.
Asili ya vazi hili ni nchi za uarabuni, dubai,turki,oman,saudia na kwa hapa Tanzania vazi hili limeshamiri sana Zanzibar nk Japo kwakipindi hichi cha hivi karibuni vazi hilo limekuwa halinamwenyewe yaani watu wote wanavaa tuseme tuu ndio imekuwa habari ya mjini kwa wanawake kwasasa.
Mwanzo vazi la abaya lilionekana ni vazi la waarabu peke ake na waislam ila kama unavyojua maisha yanaenda kwa kasi sana kutokana na utandawazi kukua kwa kasi na vazi hilo la kiislam kuvaliwa na kila mtu kutokana kukupa muonekano mzuri wa stara.
Vifaa vinavyo tumia kukamilisha vazi la abaya
-vitambaa vya hariri
-nakishi nakshi za urembo
-uzi, vifungo
Vazi hilo siku hizi hushonwa kwa kutumia cherehani, kabla halijakuwa rasmi duniani watu walikuwa wakinunua madukani tena kwa bei kubwa husani bara la Afrika, lakini kwasasa tunaweza kusema limekuwa ni rahisi kwa kiasi chake na kupelekea baadhi ya watu kuaford.
Kwa mafundi cherehani wa mtaani wamekuwa wakiyashona kwa bei ambayao inalingana na mazingira ya eneo tena kwa kipindi hichi cha mwezi wa mtukufu wa Ramadhani, vazi hili limekuwa likipendwa na waislamu wengi kwaajili ya kujistiri. Sio hivyo tu vazi hilo lina mishono tofauti tofauti na mitindo yake utofautiana kila iitwapo leo mitindo ya vazi hilo hubadilika kutokana na wakati.
Vazi hili bwana ukilivaa ili uweze kuonekana katika muonekano mzuri lazima lishonwe katika ustadi mzuri na kwa mafundi walio bobea katika ushonaji sasa wewe peleka kwa fundi Juma akikuharibia usije kulalamika, na ndio maana watu wengi hupenda kununua dukani wakati mwengine huagiza nje ya nchi mfano Dubai and Turk.
Basi bwana team ya Mwananchi Scoop tukaona isiwetabu wacha tukusogezee wafanyabiashara watakaotujuza kuhusiana na biashara hiyo gharama zake, kuelekea sikukuu za idi, wateja wakoje changamoto nk.
Tuliweza kuzungumza na Mohammedi Akida mfanyabiashara wa mavazi ya abaya, tumezoea kuona mabinti ndo hupendelea sana kuuzwa na wadada lakini kijana huyu yeye alieleza kuwa siku hizi hakuna biashara wala kazi ya kike wala kiume yeye anafanya kwa ajili ya kujipatia kipato.
Tulimuuliza kuhusiana na biashara yake huwa anapata wateja wapi na kueleza kuwa “mimi huwa natangaza biashara yangu kupitia mtandao wa kijamii kama unavyojua kipindi hichi watu wengi wanauhitaji ya mavazi hayo kwangu mimi haina ugumu sana” amesema Mohammed
Aidha tulizungumza nae kuhusu bei na biashara ikoje na kueleza kuwa “kama tunavyojua sasa hivi biashara hii imepanda kidogo so abaya zinaanzia shilling elfu 60 mpaka laki na 20 na bei hii ni kutokana na sehemu nilipochukulia abaya hilo, na wateja wananunu kwakuwa wanahitaji” amesema Akida
Kijana huyo pia ameeleza kuhusiana na bidhaa zake mahari anapochukulia na kusema kuwa yeye huwa anaagiza Dubai na Oman, kupitia kwa wafanyabiashara wakubwa wanaokwenda nchi hizo ndo anawaagiza.
Kama ilivyoada katika kila biashara kuna changamoto nayeye alifunguka na kusema kuwa “changamoto kubwa ni mzigo kugharimu pesa kiasi cha pesa kingi na wakati mwingine mzigo unaweza kuwa umeshafika lakini si ule uliouagiza” amesema Mohammed
Hatukuishia hapo bwana safari ikaanza moja kwa moja mpaka bungoni kwa mfanyabiashara mwingine Fatma Hamidu maarufu kama Fatuma collection kwa upande wake ameeleza kuwa wateja wamekuwa wakilalamika kuhusiana na bei ya abaya zake kuwa ghali, lakini mwenyewe ameeleza kuwa yeye hutoa nguo hizo Turki na Dubai ndo maani zinabei mno.
“Mimi biashara yangu ni quality ndio maana bei zangu zina kuwa juu kidogo ukilinganisha na wafanya biasha wengine lakini kwa kipindi hiki kuelekea sikukuu imekuwa sivyo na matarajio yangu kutokana na kuwepo kwa wafanyabiashara kuwa wengi wanao uza abaya siku hizi faida ina patikana japo sio kwa ukubwa huo” amesema Fatma
Haya sasa kwa upande wa bei yeye bwana, bei zake zimechachuka kidogo sio kama zile za bwana Mohammed “ mimi kama nilivyosema nguo zangu huwa zinatokea Turki so lazim ziwe na bei kama mnavyojua, bei zangu zinaanzia Laki na 50 mpaka laki mbili hii ni kutokana na ubora wake” amesema miss Hamidu
Alooooh! Nasemaje nasemaje unaanzaje kupitwa na hiki kitu mwanamke wa kileo yaani habari ya mjini ni Abaya yaani watu wameshasahau kuhusu vijora, gubeli na madera so niwakati wako sasa wewe mwanafashooni kubadilika.
Leave a Reply