Varane kuungana na Messi timu moja

Varane kuungana na Messi timu moja

Mmoja kati ya wamiliki wa klabu ya Inter Miami, #DavidBeckham imeripotiwa kuwa yupo katika mazungumzo na wawakilishi wa beki wa #ManchesterUnited, #RaphaelVarane kwa ajili ya kuipata saini yake katika dirisha hili.

Inaelezwa kuwa Miami ambayo ina mastaa kibao kama Lionel Messi, Luis Suarez na Sergio Busquets, inamtaka Varane kwa ajili ya kuboresha eneo lao la ulinzi.

Ikiwa dili hilo litakamilika Varane ambaye anawindwa na baadhi ya timu za Saudi Arabia, atakutana na Messi kwa mara yapili lakini wakati huu wakiwa timu moja.

Awali wawili hao walikuwa wapinzani walipokuwa wakicheza Hispani wakati Messi akiwa katika klabu ya Barcelona na Varane akiwa Madrid, hivyo muda mwingi walikuwa wakikabiliana uwanjani kutokana na nafasi wanazocheza.

Hata hivyo Varane anatarajiwa kuondoka Man United mwisho wa mwezi huu ambapo mkataba wake ndio utakuwa unafikia ukomo.

Beki huyu wa kimataifa wa Ufaransa, aliyejiunga na Man United mwaka 2021 akitokea Real Madrid kwa ada ya Euro 40 milioni , msimu uliyopita alicheza mechi 32 za michuano yote na kufunga bao moja akiiwezesha timu hiyo kushinda kombe la FA.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags