Vanessa Mdee afanyiwa upasuaji wa jicho

Vanessa Mdee afanyiwa upasuaji wa jicho

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva nchini ambaye kwasasa anaishi Marekani na mpenzi wake Rotimi ameweka wazi kuwa amefanyiwa upasuaji (Surgery) wa jicho na kuwa kwa sasa anaendelea vizuri.

Vanessa ameweka wazi suala hilo kupitia ukurasa wake wa TikTok kwa ku-share video akiwa na Rotimi wakicheza kwa furaha huku video hiyo ikiwa na maandishi ya kumshukuru mungu kwa upasuaji wake kwenda salama.

Utakumbuka kuwa mwaka 2019 Vanessa aliweka wazi kuwa jicho lake moja linashida ya kutokuona hivyo amekuwa akitumia jicho moja kwa takribani miaka sita.

Vanessa Mdee aliweka wazi suala hilo wakati alipokuwa Jaji kwenye mashindao ya ‘East Africa Got Talent Show’ 2019 alipokuwa akimtia moyo mshiriki aliyuekuwa na matatizo ya macho.

Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amewahi kutamba na vibao vyake kama ‘Cash Madame’, ‘Juu’, ‘Come Over’ ‘Kisela’ na nyinginezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags