Vanessa anunuliwa nyumba ya Bilioni 1.1

Vanessa anunuliwa nyumba ya Bilioni 1.1

Msanii wa muziki nchini Tanzania, Vanessa Mdee amethibitisha kununuliwa nyumba ya kifahari na mpenzi wake ambaye ni Star wa muziki nchini Marekani anayefahamika kwa jina la Rotimi.

Vanessa amethibitisha hilo akiwa kwenye podcast na mtangazaji Lilommy ambapo amesema kuwa amenunuliwa nyumba hiyo katika siku ya Valentine day huku ikidaiwa kuwa imegharimu kiasi cha Dola za Marekani 500k sawa na Bilioni 1.1 za kitanzania.

Inadaiwa kuwa jumba hil la kifahari lililopo Florida karibu na Disney World lina jumla ya vyumba sita, mabafu matano na sehemu  kubwa na kukaa.

Hata hivyo baadhi ya mashabiki wa Vanessa wameonesha kufurahishwa na kitendo kilichofanywa na Rotimi na kuwaombea Mugu wadumu milele.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags