Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na U.S. National Institute of Environmental Health Sciences (NIEHS) unaeleza kuwa asilimia 10 ya wanaume wanasumbuliwa na changamoto ya uzito mkubwa.
Utafiti huo kwa upande wa wanaume unaeleza kuwa, uzito mkubwa huhusishwa na kupungua kwa vichocheo vya kiume, mbegu za kiume dhaifu, pamoja na kupungua kwa uwezo wa kurutubisha yai la mwanamke.
Dk Mkeyenge anashauri kwa mtu anayetaka kuepuka uzito kupita kiasi ni vyema kuhakikisha anapunguza tabia ya ulaji wa hovyo na usiozingatia mlo kamili pamoja na kufanya mazoezi angalau dakika 30 kwa siku.
“Mirija ya uzazi inaweza kusababisha kuziba kwa sababu mbalimbali hivyo mayai hushindwa kupita na kusababisha ugumba”anasema
Tatizo hilo pia wakati mwingine huweza kusababishwa na magonjwa mengine ya mwili, ambayo wakati mwingine huingilia mfumo wa homoni za uzazi ikiwemo magonjwa ya kisukari na ini” alisema Dk Mkeyenge.
Leave a Reply