Uwoya agoma kufuta tatoo hadi Roho Mtakatifu amwambie

Uwoya agoma kufuta tatoo hadi Roho Mtakatifu amwambie

Mwigizaji Irene Uwoya amesema licha ya kuingia kwenye maisha ya wokovu hawezi kufuta tatoo zilizopo mwilini mwake hadi Roho Mtakatifu atapomwambia.

Uwoya ameyasema hayo leo Septemba 7, 2024 wakati akizungumza na Mwananchi katika tamasha la Faraja ya Tasnia lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam.

"Sisi binadamu tunaishi, mambo ni mengi hapa duniani unapoamua kujikataa na kumfuata Mungu siyo jambo dogo. Linachukua muda hata mimi kuna muda nashindwa, naona kama nakata tamaa lakini maombi ndiyo silaha,"amesema.

Mbali na hayo amezungumzia kilichofanya akae kimya kwa muda mrefu bila ya kuonekana kwenye kazi yoyote hadi sasa alipoibuka katika tamthiliya ya 'Mzani wa Mapenzi'.

“Mambo tu yamekuwa mengi yakawa yanaingiliana hapa na pale lakini wakanihitaji kwenye uhusika wa mapenzi nikaona why not na ndiyo kazi yangu,” amesema Uwoya

Hata hivyo katika upande wa kuokoka kwake amesema ameamua kumtumikia Mungu mpaka pale atakapomchukua.

“Nataka nisema kwamba nimeamua kuwa huku maisha yangu yote mpaka pale Mungu atakapo nichukua kwa sababu amekuwa muaminifu sana kwangu amenitendea mambo mengi sana,” ameongezea Uwoya

Aidha hakuacha kuwatoa wasiwasi baadhi ya watu wanaoamini kuwa huenda akaachana na wokovu kwa siku za mbeleni.

“Ninachoweza kusema ni kwamba siyo kitu chepesi wala kirahisi kwa hiyo kuingia na kutoka ni kawaida sana unajua sisi ni binadamu tunaishi duniani mambo ni mengi, unapoamua kukataa maisha yako na kumuamini Mungu siyo jambo rahisi ni jambo ambalo linachukua muda shetani naye ni kitu ambacho hakipendi wala hakikubali utapata vita nyingi sana,” amefunguka Uwoya

Amesema anatamani kujiona mbele zaidi katika kumtumikia Mungu hatamani kumkosea

“Natamani kujiona mbele zaidi sitamani kabisa kumkosea Mungu na sitamani kitu chochote kitakacho nikosanisha na Mungu kama kipo basi akichukue hata kama ni mali ziende tuu ili niwe karibu na Mungu.

"Kujiona niko wapi sijui Mungu mwenyewe anajua wapi ananipeleka, yeye anajua zaidi niacho amini kwamba nampenda sana na nimeamua kuwa karibu yake kutoka moyoni mwangu,” amesema Uwoya






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags