Uvaaji wa bangili za culture unavyoongeza mvuto zaidi

Uvaaji wa bangili za culture unavyoongeza mvuto zaidi

Naam!! nikukaribishe tena kwenye magazine yetu ya Mwananchi Scoop katika segment yetu pendwa ya Fashion kama kawaida yetu hapa lazima tuangazie urembo na mitindo mbalimbali.

Leo katika Fashion tutazungumzia jinsi gani uvaaji wa bangili za Culture unavyoongeza mvuto zaidi katika muonekano wako.

Bangili ni kitu kilichotengenezwa kwa ajili ya kuvaliwa mkononi nakuongeza mvuto kwa mrembo zipo aina mbalimbali za bangili za utamaduni ambazo zinatumia shanga za kimasai zingine hutumia madini kama dhahabu na mengineyo.

Bangili unayotaka kuvaa inategemea na nguo ambazo unataka kuvaa kwani kuna wale ambao wanapenda  kuvaa bangili zilizotengenezwa kwa malighafi kwa ajili ya kuendana, wengine hupendelea bangili zilizotengenezwa na vitu vya asili kama vifuu vya nazi inaaminika bangili zilizotengenezwa na vifuu vya nazi zimekuwa zikipendeza kuvaliwa kutokana na muonekano wake  na gharama yake ni nafuu.

Uvaaji wa bangili pia unatakiwa kuzingatia rangi ya mvaaji kama mtu ni mweusi anashauriwa kuvaa bangili zenye mng'ao ili kuweza kuwa na muonekano mzuri zaidi

Ni vyema kama utazingatia mpangilio wa rangi katika uvaaji wa bangili na itapendeza kama uvaaji huo utazingatia nguo uliyovaa, viatu au mkoba na hereni.

Siku za hivi karibuni mambo yamebadilika sana Fashion ya bangili imerudi kwa kasi sana, kwa sasa vijana wanapendelea kuvaa bangili za ‘Culture’ hizi ni zile bangili ambazo mwanzo zilikuwa zinaonekana na jamii ya Wamasai zikivaliwa na wanawake kwa wanaume ila sasa hivi imekuwa tofauti kutokana na utandawazi na upana wa fashion ulimwenguni.

Vijana wa kileo wamekuwa wakivaa bangili hizo za culture kama fashion tofauti na zamani hiyo ilikuwa ni tamaduni ya Wamasai na baadhi ya makabila Afrika.

Hivyo basi Mwananchi Scoop ilikutana na mwanamitinndo wa kutengeneza bangili za culture, Peragia Daniel anatufafanulia jinsi gani bangili za ‘culture’ zinavyopendwa na watu kwa sasa na imekuwa moja ya urembo ambao lazima mtu atakuwa nao mkononi si mwanamke wala mwanaume.

“Bangili za culture zimekuwa ni fashion inayokuja kwa kasi ulimwenguni kwa sababu zinapendwa na watu wa rika zote hususani vijana wa kileo wanaoenda na fashion.

Mwanzoni nilianza na kutengeneza ilikuwa ngumu sana watu kuelewa lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda mambo yanakuwa tofauti, baada ya watu wa ughaibuni hususani wazungu wanaokuja kutalii Tanzania kuanza kuvutiwa na aina hii ya bangili.

 Basi nao vijana Wakitanzania wakaona kumbe hii nayo ni fashion hapo sasa nikanza kuona ‘oda’ za vijana wengi wakiagiza ni wabunie.” Alisema Pelagia

Pia mwanadada huyo ameeleza kuwa aina ya bangili hizo zipo za kike na za kiume kwa nakshi tofauti tofauti na gharama ya ununuaji wa bangili hizo ni tofauti na bangili nyengine tulizo zizoea anasema.

“Bei ya bangili hizi inamfaa kila mtu kwa sababu azina bei kubwa kama tulivyo kwa bangili nyingine na ndiyo maana mimi huwa nikitengeneza hazikai muda mrefu zinaisha na material yake ni rahisi kupatikana tena kwa bei nafuu hivyo huwa hainipi shida”

Haya sasa hayo ndiyo mambo ya Fashion, yaani kisicho kufaa leo kwenye fashion baada ya miaka kadhaa kinakuwa ndiyo habari ya mjini katika mitindo, hivyo basi hatukuishia hapo moja kwa moja mpaka kwa mrembo, Tausi Ramadhani mkazi wa Dar es salaam yeye anatueleza ni jinsi gani anavyovutiwa na bangili za ‘culture’.

“mimi huwa napenda sana bangili za ‘culture’ tena huwa navaa pamoja na saa huwa inaleta muonekano mzuri katika mkono wangu na huwa ni bangili ambazo hazina mambo mengi kwa sababau siyo za chuma material yake ya shanga kama Wamasai hivi yani ukivaa unatokelezea” alisema Tausi.

Pia naeleza kipindi cha nyuma hakuweza kuzielewa bangili hizo ila alipoona kwa marafiki zake wanavaa bangili hizo na ziliwapendeza hakuwa na budi na yeye kuiga Fashion hiyo ambayo kila mtu anaipenda kwa sasa.

“Kiukweli kwa sasa kama kuna watu hawavai  ‘culture’ mkononi mwake basi itakuwa ni wachache, mwanzo mimi sikuwa naipenda sana aina ya bangili hiyo ya ‘culture’ lakini kunasiku niliona kwa marafiki zangu chuoni ziliwapendeza sana nikatamani na mimi nikasema hii fashion haiwezi kunipita kabisa” alisema Tausi

Haya sasa na wewe unaanzaje kupitwa na urembo kama huu ambao sasa umekuwa habari ya mjini kila unapopita kila mtu utaona amevaa bangili aina ya ‘culture’ mkononi halafu unaweza ukabebeshea na saa na ikawa na muonekano mzuri mkononi mwako.

Haya mimi kwa leo katika ulimwengu wa Fashion yangu yalikuwa ni hayo tukutane tena next week katika ulimwengu wa Fashion ambao utaikuta katika magazine yako pendwa ya Mwananchi Scoop.

Hii imeenda mwanetu!!!!!

.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags