Utanashati ulifanya mjukuu wa Mwaikibaki akose pesa

Utanashati ulifanya mjukuu wa Mwaikibaki akose pesa

Mwanamitindo na mfanyabiashara ambaye pia ni mjukuu wa Hayati Mwaikibaki, Sean Andrew, amefunguka na kuweka wazi kuwa aliwahi kukataliwa kufanya tangazo kisa utanashati (uzuri) aliokuwa nao.

Sean ameyasema hayo katika mahojiano yake na podcast ya Flo & Frens baada ya kuulizwa kuhusu faida na hasara za kazi yake ya mwanamitindo na kueleza kuwa aliwahi kukataliwa katika dili la kufanya tangazo kwa kuwa na muonekano mzuri (handsome).

Ambapo wahusika wa tangazo hilo alilogoma kuwataja walimpigia simu na kumwambia yeye ni mzuri sana hivyo walitaka mtu mkakamavu.

Kwa mujibu wa mwanamitindo huyo alieleza kuwa aliamini kupitia kampuni hiyo ingeweza kumchagua jambo ambalo lilikuwa kinyume. Amedai kuwa tukio hilo lilimkatisha tamaa kwa sababu aliweka matumaini makubwa katika tangazo.
.
.
.
#MwananchiScoop.
#Burudika






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags