Kwa mujibu wa utafiti mpya uliofanywa kutoka Chuo Kikuu cha Texas huko Austin unaeleza kuwa watu wapweke na wenye mfadhaiko (depression) wanaongoza kutazama televisheni kupita kiasi.
Hata hivyo utafiti huo unaeleza kuwa watu hao watazamao vipindi vya televisheni mfululizo hufanya hivyo kwa lengo la kuwaepuka watu wanaowafanya wapate mfadhaiko (depression).
Aidha watafiti hao wame watahadhalisha watu hao kwani kufanya hivyo kunasababisha matokeo mabaya kama vile kukosa usingizi, kuongeza hisia za kutendwa na kuzidisha matatizo ya msingi ya upweke na mfadhaiko.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply