Utafiti waonesha kucheka ni matibabu ya moyo

Utafiti waonesha kucheka ni matibabu ya moyo

Utafiti uliofanyika nchini Brazili umegundua kuwa kucheka kunasaidia katika matibabu ya ugonjwa wa moyo kwa asilimia 10.

Utafiti huo uliofanywa na Hospitali ya Clinicas de Porto Alegre ukiongozwa na Daktari bingwa wa moyo, Profesa Marco Saffi uligundua kuwa tiba ya kucheka inaweza kusaidia kupunguza uvimbe katika mishipa ya moyo na kupunguza hatari ya mshtuko wa moyo na kiharusi.

Wanasayansi nchini Brazili walifanya jaribio la kuchunguza ikiwa 'matibabu ya kucheka' yanaweza kuboresha dalili za moyo na mishipa.

Utafiti huo ulioitwa ‘Tiba ya kicheko’ umebaini kuwa kucheka kunaweza kusaidia moyo kwa sababu hutoa ‘endorphins’, ambayo hupunguza uvimbe na kusaidia moyo na mishipa ya damu kufanya kazi vizuri.

Pia hupunguza viwango vya homoni za sonona, ambayo huchangia kuwa na uvimbe katika moyo.Hospitali hiyo, ilifanya uchunguzi kwa wazee 26 wa miaka 64 wenye matatizo ya moyo ambao baada ya kuwekewa programu ya vichekesho kila wiki walipata ahueni na uvimbe katika mioyo yao ulipungua.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags