Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida la ‘Archives of Behavior’ umebaini kuwa wanaume wenye ndevu ni waaminifu huku wakiripotiwa kudumu kwenye mahusiano na mpenzi mmoja bila ya kutafuta mchepuko au mpenzi mpya.
Utafiti huo uliyofanywa kwa wanaume wenye umri wa miaka 18 hadi 40 ulibaini kuwa wenye ndevu walionesha kulinda mahusiano yao na kujali familia huku wasio na ndevu walionekana kulenga zaidi katika kutafuta wapenzi wapya.
Aidha Profesa Peter Jonason kutoka Chuo Kikuu cha Cardinal Stefan Wyszynski cha Warsaw aliwahi kusema kuwa kutanza ndevu kunaweza kuashiria nidhamu na utulivu.
Leave a Reply