Utafiti: Nusu ya vijana wenye miaka 18 hadi 29 wanaishi kwa wazazi

Utafiti: Nusu ya vijana wenye miaka 18 hadi 29 wanaishi kwa wazazi

Kutokana na utafiti uliofanywa mwaka jana  na kituo cha Pew Research, umegundua kuwa karibia nusu ya vijana wote nchini Marekani walio na umri kati ya miaka 18 hadi 29 bado wanaishi na wazazi wao.

Sababu kubwa ya hali hiyo inatajwa kuwa ni tatizo la kiuchumi, huku gharama za kukodisha nyumba zikielezwa  kuongezeka, hivyo vijana wanalazimika kukaa nyumbani kwa ajili ya kutunza pesa za kujiandaa na maisha ya kupanga baadaye.

Pia sababu nyingine imetajwa kuwa baadhi yao hupenda kuishi na wazazi wao kwa ajili ya kupanga vizuri bajeti zao kwa matumizi yao binafsi kama vile usafiri na kufanya anasa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags