Utafiti: Mabishano ya utotoni yanafaida ukubwani

Utafiti: Mabishano ya utotoni yanafaida ukubwani

Kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa na Chuo Kikuu cha Cambridge umebaini kuwa ugomvi wa watoto waliofuatana unaweza kuwanufaisha hapo baadaye.

Utafiti huo uligundua kwamba mabishano ya utotoni kati ya ndugu yanaweza kuboresha ujuzi wa kijamii, msamiati, maendeleo, na kwa kiasi kikubwa unawanufaisha watoto hao.

Profesa Claire Hughes, ambaye ni mmoja wa waandishi wa utafiti huo ameeleza kuwa migogoro hiyo huwasaidia watoto kujifunza ujuzi muhimu wa kijamii huku akitaja kuwa mtoto wa pili kuzaliwa ndiyo hufanya vizuri kwenye masomo yake.

Utafiti huo, ambao uliwafuatilia watoto 140 kwa miaka mitano, pia ulionesha kwamba ingawa mizozo ya kawaida ni yenye manufaa, lakini ushindani wa kudumu unaweza kusababisha matatizo ya kitabia yasiyokwisha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post