Utafiti: Kuoga hakuna faida yoyote kwa afya

Utafiti: Kuoga hakuna faida yoyote kwa afya

Inadaiwa kuwa tabia ya kuoga kila siku haina faida yoyote kwa afya ya binadamu, bali watu hufanya hivyo, wakihofia kutengwa na jamii, kwa sababu ya kunuka.

Kwa mujibu wa tafiti za wataalamu wa Afya akiwemo Julie Russak, ambaye ni Daktari wa Ngozi, huko Manhattan, nchini Marekani ameeleza kuwa tabia ya kuoga mara kwa mara, inaweza kuondoa bakteria wa ulinzi wanaokaa kwenye ngozi ya mwanadamu.

Pia mtaalamu wa masuala ya Kemia nchini humo, David Whitlock, ambaye aliacha kuoga kwa muda wa miaka 12 na kuchagua kujipulizia manukato yenye mchanganyiko wa bakteria wa ulinzi wa ngozi, aliwaasa watu kuacha kuoga ili kuwalinda bakteria hao muhimu kwa afya ya binadamu.

Je unaweza kuishi bila kuoga na kutegemea manukato pekee kama mbadala wa kuoga?
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post