Usher ataka Kolabo na Nandy

Usher ataka Kolabo na Nandy

Baada ya kufanya ‘kolabo’ ya ngoma yake inayotrend kupitia mitandao ya kijamii ya ‘Dah’ na Alikiba mwanamuziki Nandy ameweka wazi kuwa msanii kutoka nchini Marekani Usher anataka kufanya ‘kolabo’ ya ngoma hiyo.

Nandy kupitia ukurasa wake wa instagram ame-share chati zake na Usher ambapo msanii huyo alieleza kuwa ameukubali wimbo huo hivyo basi anahitaji kuweka verse yake katika ngoma hiyo.

Remix ya wimbo wa ‘Dah’ ambao alimshirikisha Alikiba bado unaendelea kushika namba moja kupitia mtandao wa YouTube ukiwa na Zaidi ya watazamaji milioni 2 ndani ya siku tano tuu tangu kuachiwa kwake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags