Usher ataja sababu ya kuhairisha show

Usher ataja sababu ya kuhairisha show

Mwanamuziki wa Marekani Usher Raymond ametaja sababu ya kuhairisha ziara yake ya kidunia ya ‘Past, Present, Future’ aliyotakiwa kuifanyika jana Jumatatu jijini Atlanta.

Kufuatia na taarifa aliyoitoa katika ukurasa wake wa Instagram ameweka wazi kua amechukua uamuzi huo kutokana na kutokuwa sawa kimwili hivyo anahitaji kupumzika ili kurudi tena jukwaani akiwa na nguvu asilimia 100.

“Kwa miaka yangu zaidi ya 30 ya kazi, asilimia 100 ya damu yangu, jasho, na machozi imeenda katika kutoa maonyesho bora zaidi na kuunda uzoefu wa kukumbukwa kwa mashabiki wangu, Nina nia kamili ya kufanya hivyo kwa ziara hii pia, ndiyo sababu lazima niahirishe onyesho la usiku wa leo.

“Jambo la mwisho ambalo ningependa kufanya ni kutowaangusha nyinyi, mashabiki ambao mmekuwa mkisubiri kwa hamu ziara hii ianze. Hata hivyo, nisingekuwa msanii niliye kama siwezi kuwapa kile bora zaidi kimwili” Ameandika Usher



Aidha kwa sasa maonesho yake mengine mawili yaliyopangwa kufanyika Ijumaa na Jumamosi State Farm Arena yatafanyika kama kawaida huku onesho lililohairishwa jana likitarajiwa kufanyika Novemba 30 mwaka huu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags