Usher amtaka mwanawe aingie kwenye muziki

Usher amtaka mwanawe aingie kwenye muziki

Mwanamuziki wa Marekani, #UsherRaymond amemtaka mwanawe wa kiume aitwaye Naviyd aingie kwenye muziki mapema na kujisimamia mwenyewe akiwa na umri wa miaka 15.

Inaelezwa kuwa Usher mwenye umri wa mika 45 ameyasema hayo week iliyopita wakati wa sherehe ya tuzo za ‘Voice of the Culture Award’ ASCAP iliyofanyika nchini Uingereza.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali zinaeleza kuwa msanii huyo amemuhimiza mwanawe kuingia katika muziki akidai ameweza kuhakikisha Naviyd anakuwa ana mwanzo mzuri katika safari yake ya muziki kwa kumpa mafunzo bora.

 Hata hivyo Usher amesema kuwa alifurahishwa sana kwa watoto wake wawili, Naviyd na Cinco kwenda kushuhudia akipata tuzo ya utunzi bora wa nyimbo na utayarishaji katika sherehe hiyo.

Usher mwenye mafanikio makubwa katika muziki amebahatika kupata watoto wa wanne akiwemo Cinco V,  Naviyd, Sovereign Bo na Sire Castrello.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags