Usher ampa shavu Burna Boy

Usher ampa shavu Burna Boy

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria #BurnaBoy amepewa shavu na mwananuziki wa Marekani Usher kwa kushirikishwa kwenye albamu yake iitwayo ‘Coming home’ inayotarajiwa kutoka siku ya Ijumaa, Februari 9, 2024.

Albamu hiyo ina nyimbo 20, ambapo Burna Boy ameshirikishwa kwenye wimbo wa kwanza uliobeba jina la albamu, pia wasanii wengine walioshirikishwa ni 21 Savage, Summer Walker na Phelz.

Usher hadi sasa ana jumla ya albamu 25 ambazo alizitoa miaka tofauti, ikiwemo ‘Live’ (1999), ‘May Way’ (1997), ‘I wanna be’ (2015), ‘chatt Town’(2012), ‘The groove’(2014).

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Burna kushirikishwa na msanii mkubwa kutoka Marekani, pia amewahi kufanya kazi na 21 Savage wimbo 'Just Like Me (2024)', Jon Bellion 'I Feel It (2022)', Becky G 'Rotate (2021)', Sam Smith 'My Oasis (2020)', IDK 'December' (2019)' bila kusahau nwimbo wake 'For My Hand (2023)' aliyofanya na Ed Sheeran.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags