Upikaji karanga za mayai

Upikaji karanga za mayai

Habari kijana mwenzangu mwanaharakati ukiwa umetulia unafikiria kuna dili amabalo linaweza kukutoa ukapata shilingi mbili tatu?, leo nakupa dili hili hapa la utengenezaji wa karanga za mayai hakika ukifuzu kutengeneza tayari umeshatoboa mwanangu.

Hivyo ungana nami twende sawa kwa kuangalia mahitaji ya awali kabla ya kuanza kukaanga karanga za mayai, zingatia kwa makini kabisa ili uweze kufanikiwa zaidi karibu.

Mahitaji

  • Sukari kiasi
  • Unga wa ngano kilo  moja na nusu.
  • Karanga kilo 1
  • Mayai 3
  • Mafuta ya kupikia kiasi kulingana na mchanganyiko wako.

Namna ya kutengeneza

  • Pasua mayai ,changanya mayai na sukari kisha koroga katika chomba kimoja.
  • Hatua ya pili chukua unga wa ngano kisha changanya na mchanganyiko wa mayai na sukari.
  • Weka mafuta katika sufuria kisha injika jikoni, Lakini hakikisha moto hauwi mkali sana, Ukiwa mkali sana utasababisha karanga kuungua sana na kupoteza ladha.
  • Koroga mchanganyiko huo taratibu ili kuondoa kugandamana kwa mchanganyiko huo wa karanga pamoja na unga wa ngano, Fanya hivyo kila baada ya dakika kadhaa.
  • Ukiona zimeanza kubadilika rangi onja kwa kujiridhisha kama kweli zimeiva.
  • Zikisha iva ziepue kisha weka katika chombo kisafi ili zipoe, Baada ya dakika kadhaa zifunge katika vifungashio kwa ajili ya biashara.
  • Mimi nakupa mchongo unaweza fanya hivi kwa mtaji wako mdgo sana na ukaweza kuingiza faida usiwe na tamaa kwa kuweka bei kubwa ukakosa wateja weka bei ambayo watu wataimudu au sio?.

Hakikisha unatengeza karanga zenye ubora ambazo wateja watavutiwa nazo nakutakia utafutaji mwema na pambana kadri uwezavyo siku njema mdau.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post