UN yaitaka FIFA kutoa malipo sawa, wachezaji wa kike na wakiume

UN yaitaka FIFA kutoa malipo sawa, wachezaji wa kike na wakiume

Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) limeshauri Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kuhakikisha linatoa malipo sawa ya fedha na tuzo kwa wanawake , kama ilivyo kwa wanaume hadi kufikia Kombe la Dunia la Wanawake Mwaka 2027.

Raisi wa FIFA Gianni Infantino aliwaomba wafadhili kuwekeza zaidi ‘soka’ la wanawake.

Amesema kuwa suala la usawa ni gumu kufikiwa japo kuwa nia yao ni kuhakikisha unakuwepo katika Kombe la Dunia la Wanaume 2026 na Kombe la Dunia la Wanawake 2027.

2023, fedha na tuzo zilizotolewa kwenye Kombe la Dunia la Wanawake ni takriban Tsh. Bilioni 275.5, wakati ‘timu’ za Wanaume zilizocheza Fifa World Cup2022 Qatar zilipewa takriban Tsh. Trilioni 1.1






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags