Umuhimu wa vyama vya wafanyakazi

Umuhimu wa vyama vya wafanyakazi

Na Habiba Mohammed

Yes, karibu sana kwenye makala za kazi, ujuzi na maarifa. Swala la vyama vya wafanyakazi limekuwa changamoto kwa waajiriwa katika sehemu zao za kazi.

Mwananchi Scoop katika makala ya kazi tunaekuelezea umuhimu wa vyama vya wafanyakazi katika maeneo ya kazi. Fuatilia kwa undani uweze kujifunza zaidi.

Kulingana na sheria ya ajira na mahusiano ya kazi, chama cha wafanyakazi ni idadi yoyote ya wafanyakazi inayohusiana pamoja kwa madhumuni, ikiwa kipekee au kwa madhumuni mengine ya kusimamia mahusiano kati ya wafanyakazi na waajiri wao, aidha mashirika ya waajiri ambayo waajiri wao ni wanachama vilevile ili vyama vya wafanyakazi viweze kutimiza majukumu yake lazima muajiri akubali uwepo wa vyama hivyo katika shirika au kampuni yake na ikiwa na sheria na kanuni zilizopo pia vyama hivi ni hiari kujiunga.

Vyama vya kazi vinavyotambulisha waajiri hujulikana kama TUCTA (Trade union congress of Tanzania) na wajiriwa hutambulishwa na TUGHE (Tanzania Union of Government of Health Employees).

Ufuatao ni umuhimu wa vyama vya wafanyakazi

  • Vyama vya wafanyakazi ni kutetea na kulinda maslahi ya wafanyakazi kwa waajiri wao, kwani chama humtambulisha mfanyakazi katika majadiliano ili kupata stahiki bora kazini mfano maswala ya likizo (martenity leave, sick leave), ongezeko la mishahara n.k.

 

  • Kutoa elimu kwa waajiri na wafanyakazi kuhusiana na afya na usalama katika mazingira ya kazi kwa mfano taasisi ya OSHA pia kuboresha uhusiano wao katika mahali pa kazi.

 

  • Inaongeza ushirikiano na umoja kati ya mwajiri na mfanyakazi katika ufafanuzi wa sheria elekezi za nchi ili kuboresha utendaji wao wa kazi na ufanisi na tija ili kuwepo na urahisi katika uandaaji wa mikataba ya hali bora.

 

  • Husaidia kupunguza migogoro katika katika eneo la kazi kati ya mwajiri na mwajiriwa kupitia sheria za vyama zilizopo zinazo muongoza mujiari.

 

Licha ya vyama vya wafanyakazi kuwa na umuhimu katika mahali pa kazi vilevile vina jukumu la kuhamasisha usawa wa jinsia katika maeneo ya kazi na kutoa kipao mbele kwa sekta zisizo rasmi kujiunga na kuunda vyama vya wafanyakazi katika kutetea na kulinda maslahi yao.

Aidha, mfanyakazi mpya anatakiwa kujua nature or history ya taasisi au kampuni anayoifanyia kazi kama inaruhusu uwepo wa vyama vya mfanyakazi, pia mfanyakazi anatakiwa kujua uongozi au viongozi ambao ni wawakilishi kutoka kwenye vyama vyao. 

Vilevile vyama vya wafanyakazi vina jukumu la kutokomeza ajira za utotoni katika maeneo ya kazi, kuboresha ufanisi kazini kwa kuzingatia masaa ya kazi kwa wafanyakazi, afya na usalama wao.

Mfanyakazi atanufaika akijiunga na vyama vya wafanyakazi kwani atakuwa na ‘greater bargaining power for defending his or her own interest’ lakini pia husaidia kuongeza usawa katika fursa mbalimbali kwa jinsia zote mbili, kuongeza ushiriki na ushirikishwaji wa wafanyakazi n ahata usalama wa kazi yako kwa mfano wafanyakazi kupunguzwa kazini kutokana uchumi wa kampuni kushuka au mlipuko wa magonjwa hatarishi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags