Umuhimu wa ushirikiano kazini

Umuhimu wa ushirikiano kazini

Heyy! I hope mko poa wanangu sana sisi tunakwambia mwendo ni ule ule wa back to back kila weekend lazima tuwaelekeze nini kimejiri, katika segment yetu ya kazi.

Leo katika kazi tutakueleza faida na umuhimu wa kushirikiana katika ufanyaji kazi katika kampuni husika

Kwanza kabisa kumekua na malalamiko baina ya wafanyakazi kwa wafanyakazi au boss na watu anaowasimamia kutokana na kukosa ule muunganiko ama ushirikiano katika masuala ya kikazi.

Nikwambie tu kwamba ushirikiano katika sehemu za kazi unaweza kuleta tofauti kati ya mafanikio na kushindwa kwa biashara nyingi.

Katika sehemu ya kazi yenye ushirikiano, watu binafsi hujihusisha kwa hiari katika mawasiliano ya wazi. Mara nyingi Wasimamizi na wafanyikazi wa ngazi ya chini hufanya kazi pamoja na kujaribu kupunguza mabishano.

Halkadhalika wafanyakazi kwa maana kwamba wanajaribu kuzuia matatizo kabla ya kupata nafasi ya kutokea.

Sambamba na hayo ushirikiano sio jambo rahisi kila wakati kufanikiwa mahali pa kazi, lakini inafaa kujitahidi kwa sababu husababisha utendaji mzuri na wenye tija.

Sasa basi twende sambamba kuangalia umuhimu wa ushirikiano mahali pakazi.

  • Kuongezeka kwa ufanisi

Kila mtu anapokuwa anafanya kazi kwa ushirikiano, kila kitu hukamilika kwa haraka na ufanisi zaidi.

Ushirikiano huokoa muda pia kwasababu wafanyakazi na wasimamizi hawahitaji kutenga muda wa kusuluhisha migogoro, pia umoja wa wafanya kazi hawa kufanya kazi zifanyike kwa kiwango cha juu sana.

 

  • Kufanya kazi bila kinyongo

Wakati mabishano na lawama zinapotawala kwenye ofisi fulani, wafanyakazi wengi huchukua uamuzi wa kuanza kazi.

Ushirikiano kazini kwa kiasi kikubwa hufanya wafanyakazi wawe na urafiki na mabosi zao kiasi cha kufanya pale linapotokea kosa, bosi aangalie namna nzuri ya kulitatua bila ya kuacha kinyongo kwa yeyote.

Mara nyingi kama hakuna ushirikiano wafanyakazi hata kama wana ugomvi huwa ni ngumu kuamuliwa na mwisho wa siku hujikuta wanafanya azi wakiwa na vinyongo moyoni hali inayosababisha muda mwingine wakipata sehemu mbadala hata kwa maslahi kiduchu waondoke ili kutafuta amani.

  • Kutoka mioyo ya wafanyakazi

Waajiriwa wanapokuwa wanafanya kazi bila ya kushirikishwa na mabosi wao hujiona kama hawana thamani na muda mwingine huona hawana mchango wowote kwenye kampuni.

Lakini pale wanapokuwa wanashirikishwa na viongozi wao kwenye masuala mbali mbali ya maendeleo ya kampuni kwa kutoa mawazo yao juu ya nini kifanyike kwenye jambo fulani, hujihisi wana thamani na wana sauti kwenye maendeleo ya kampuni husika na wanaona kwamba wana mchango mkubwa.

  • Kupunguza kutokuelewana

Katika maeneo ya kazi ambayo yanakosa ushirikiano, wafanyakazi kwa kawaida hujigawanya katika makundi. Hili linapotokea kunakuwa na kutokuelewana.

Lakini kama kutakuwepo na ushirikiano mahali pa kazi, huwa inasaidia wafanyakazi kutokwamishana kimakusudi na hali ambayo huiweka kampuni kwenye kipindi kigumu kwani kazi pia huaribika.

Kwa kumalizia, kuwa na timu yenye ushirikiano wa karibu inahitaji juhudi na nia njema kutoka kwa kila mmoja. Thamini mchango wa wenzako, jenga uhusiano wa kibinafsi, na fanya kazi kwa pamoja kuelekea malengo ya timu.

Kwa kufanya hivi, utaunda timu yenye ufanisi na furaha. Je, umekuwa na uzoefu mzuri wa ushirikiano wa karibu katika mahusiano yako ya kazi? Basi kama ni hivyo ni vyema ukaendelea na hali hiyo ya ushirikiano.

Haya sasa mwanetu hapa utakuwa umepata kitu kupitia hili ni wewe tu kuyafanyia kazi hayo yalio elezwa ili uweze kufanya kazi kwa ufanisi ukishirikiana na wanao wengine bila kinyongo wala kuwa na kauli chafu kama nilivyoeleza huko juu.

Kufikia hapo sisi hatuna la ziada tunaweka kalamu chini tukitafakari next weekend tukuwekeeni nini katika segment yetu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags