Umuhimu wa stadi za mawasiliano kwa vijana.

Umuhimu wa stadi za mawasiliano kwa vijana.

Vijana ndiyo nguvu kazi ya Taifa inayotegemewa katika kujenga jamii bora itakayokuwa imara hapo baadae, pamoja na vijana kutegemewa zaidi na serikali bado kundi hilo linakumbana na changamoto inayoikabili  dunia hivi sasa.

 

Ni wazi kuwa wanafunzi wengi wanapomaliza elimu zao au masomo yao malengo yao huwa ni kuajiriwa, huku baadhi yao wakiwa na mitazamo ya kujiari wao  wenyewe.

 

Kwa mujibu wa Shirika la Kazi duniani (ILO), tatizo la ajira  kwa vijana ni moja ya mitihani  inayoikabili dunia hivi sasa na tatizo hili linahitaji suluhu ya pamoja kuitatua changamoto hiyo.

 

Licha ya kuwepo kwa changamoto ya ajira duniani, vijana wanapaswa kutambua umuhimu wa kujifunza stadi za mawasiliano wakati wanapambana kutafuta soko la ajira.

 

Utawezaje kufikia malengo yako ya kuajiriwa kabla ya kujiajiri?

 

Stadi za mawasiliano ni mmoja ya njia ambayo kijana anaweza kutumia ili kufikia malengo yake ya kutafuta ajira katika ofisi au taasisi fulani.  

 

“Stadi za mawasiliano ni ujuzi wa mawasiliano ambao mtu anaweza kuutumia wakati wa kutoa na kupokea aina mbalimbali za taarifa au habari, vilevile ustadi huu unaweza kuwa sehemu ya kawaida ya maisha yako ya kila siku ya kazi.”

 

Ili uweze kufika pale ambapo unatarajia kufika utatumia ujuzi wako wa mawasiliano katika kila hatua ya utafutaji wa kazi na kazini, kila kitu kutoka kwa wasifu wako hadi usaili wa kazi na zaidi itahitaji aina tofauti za ujuzi wa mawasiliano.

 

Stadi za mawasiliano katika mahojiano ya kazi

 

  • Kwanza hakikisha kuwa wasifu wako umeundwa ipasavyo na hauna tahajia (spelling) na makosa ya kisarufi.

 

  • CV yako inatakiwa iwe na maelezo ya kujitosheleza, yenye kukuelezea wewe ni nani na umefanya vitu gani. Iwe short and clear!

 

 

  • Njia nyingine muhimu ambayo unaweza kuwasiliana katika mahojiano yako ni jinsi unavyojionyesha, yaani muonekano wako unaelezea taswira halisi ya kwako.

 

  • Pia Jitokeze kwa mahojiano kabla ya ule muda wa kuingia katika chumba cha mahojiano dakika 10-15 mapema na uvae vizuri kwa kazi unayoomba, na zingatia vidokezo visivyo vya maneno unavyoonyesha kupitia lugha ya mwili. 

 

  • Epuka vitendo kama vile kulala au kutazama simu yako wakati wa mahojiano, kumuangalia muulizaji wako machoni.

 

  • kutumia ustadi wa kusikiliza na kuonyesha ujasiri ni njia zote nzuri za kuwasiliana katika mahojiano yako.

 

  • Jitahidi kila unachofanya kazini na maishani vinaweza kuonekana kama njia ya mawasiliano.

 

  • Vile vile kwa kutambua nguvu na udhaifu wako na kufanya mazoea mazuri mara kwa mara, unaweza kuboresha njia unayounganisha na kuwasiliana na wengine.

 

Ujuzi wa mawasiliano kwa barua ya kifuniko (cover letter)

 

Cover letter ni fursa nzuri ya kufafanua juu ya ustadi wako wa mawasiliano. Wakati unaweza kuzungumza moja kwa moja juu ya jinsi unavyowasiliana vyema, kwa kiwango cha juu, barua yako ya kifuniko ni moja wapo ya maonyesho ya kwanza ya mwajiri juu ya ujuzi wako. 

 

Unachotakiwa kuifanya barua yako ni kuwa fupi, iliyoandikwa vizuri, isiyo na makosa ya typos na tahajia na inayolingana na nafasi unayoomba.

 

Vitu vya kuzingatia wakati wa kuandika barua pepe (email)

 

Kuwepo kwa mabadiliko ya teknolojia na hali halisi ya sasa mambo yamebadilika katika maisha ya sasa barua pepe imekuwa ni kitu cha muhimu sana, tunalazimika kuandika barua pepe katika matumizi mbalimbali ya kiofisi na binafsi, ni vigumu kukwepa matumizi ya barua pepe kwa sasa kwani ili uweze kuendelea matumizi ya barua pepe ni muhimu sana kwa kijana wa sasa.

 

  • Mstari wa somo (subject line)

Hapa unatakiwa kuandika mada inayoonyesha utayari wa kusoma kilichopo katika ujumbe wako, hakikisha mada yako ya barua pepe inaweza kumvutia mtu kama utaiweka namna ya kuvutia.

Pia hakikisha mada yako unaiandika kwa herufi kubwa na iwe yakueleweka isije ikamchanganya mtu ambae unamtumia.

 

  • Sehemu ya ujumbe(message body)

Hakikisha wakati unaandika ujumbe wako unaanza na salamu kwa ufupi, andika ujumbe mfupi, unaoeleweka  na unaoendana na mada husika.

 

  • Jitahidi kuepuka maombi/mawazo ya aina mbili katika aya moja.

 Kama umeambatanisha taarifa katika barua pepe yako, hakikisha unaziorodhesha na kumuomba msomaji azisome. Kufanya hivyo kutamshawishi msomaji kuzipitia /kuzisoma taarifa zako.

 

  • Kumbuka kuhakiki ujumbe ulioandika kabla haujafika kwa msomaji,epuka makosa ya kisafufi (grammatical error) pamoja na kukosea maneno matumizi ya R na L.

 Jitahidi pia kuhakiki barua pepe ya mpokeaji ili kuepuka ujumbe kutofika kwa mlengwa.

 

  • Ili uweze kufikisha barua pepe yako kwa mlengwa utaangalia kama wapokeaji wa jumbe hawafahamiani au kama wapo katika ofisi moja au kampuni tofauti.

Ni vyema kumtumia kila mmoja barua pepe yake bila kuwaunganisha wote katika Cc na Bcc.

 

Angalizo: Unapotuma barua pepe kwa mtu zaidi ya mmoja zingatia matumizi ya To, Cc na Bcc

 

To: ni sehemu ya kuandika barua pepe ya mpokeaji(email).

 

Cc:  ambayo ni carbon copy ikimaanisha “kupitia kwa” (sending a copy of an email to other people)

 

Bcc: ikimaanisha (Blind carbon copy) hii pia hutumwa kama copy.

Tofauti kati ya Cc na Bcc ni pale ambapo utamtumia mtu katika Bcc hatoweza kuona wenzake waliotumiwa ujumbe.

 

Hivyo basi kwa kutumia stadi za mawasiliano kunaweza kukujenga kifikra na kimtazamo pia kukusaidia kufahamu namna ya kuwasiliana na watu husasani masuala ya kiofisi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post