Umuhimu wa pochi kwa mwanamke

Umuhimu wa pochi kwa mwanamke

Habari msomaji wetu wa dondoo za fashion, ni siku nyingine tena tunakutaka hapa ili kuweza kujuzana mambo mbalimbali kuhusiana na masuala mitindo, urembo na mavazi ambayo najua unayajua ila mimi nakujua tu zaidi.

Leo kwenye masuala ya urembo tutaangalia juu ya umuhimu wa pochi kwa mwanamke.

Pochi ni sehemu muhimu sana katika maisha ya mwanamke, Pochi zipo za aina nyingi, rangi na ukubwa wa tofauti na zimekuwa na matumizi mbalimbali.

Hakika ni nadra sana kukutana na binti au mama anatembea bila pochi na wapo wengine maisha yao yote lazima watembee na pochi kwani wanaona ni kitu cha muhimu sana.

Ni kweli pochi ni muhimu katika maisha ya mwanamke kwani uhifadhi vitu mbalimbali miongoni mwa vitu muhimu ambavyo vinapaswa kukaa katika pochi ya mwanamke ni dawa yoyote ambayo unahitumia na kuihitaji, vitambulisho mbalimbali, kadi ya benki, pedi, kalamu, notebook, pini, sindano na uzi.

Aidha vipo vitu ambavyo si muhimu kukaa katika pochi lakini kama ukipenda unaweza ukaweka, vitu hivyo ni pafyumu, poda, katana, kanga, sandozi kama unavaa viatu virefu na lip stick.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags