Umuhimu wa maoni ya wateja katika biashara yako

Umuhimu wa maoni ya wateja katika biashara yako

Mambo zenu marafiki zangu na wafanyabiashara wenzangu, I hope mko pouwa kabisa, kama kawaida yetu madhumini yetu ni yale yale kuja kuelimishana na kuelezana kuhusiana na maswala mazima ya biashara na ujasiriamali.

Baadhi ya wafanyabiashara huwa wanazarau sana kipengele hichi sijajua sababu ni kitu gani, lakini leo nipo hapa kwa ajili ya kuwajuza umuhimu wa maoni ya wateja katika biashara yako.

Maoni ya wateja katika biashara ni jambo ambalo litakusaidia sana na litaweza kukuletea wateja wengi kuliko hata unavyofikiria, maoni au comment kutoka kwa wateja wako kwanza ni muhimu kuyafuatilia kwasababu ndo kitu kitakachokusaidia kujua kuwa bidhaa unazo ziuza wanazipenda au hawazielewi.

Na hizi ni baadhi ya sababu za umuhimu wa maoni ya wateja katika biashara yako…

  • KUONGEZA UTIMILIFU WA WATEJA

Kwa kusikiliza maoni ya wateja, biashara inaweza kukua na kuboresha muonekano wa bidhaa au huduma zake ili kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja, na hivyo kuongeza utimilifu wa wateja.

  • KUONGEZA USHINDANI

Biashara inayosikiliza na kujibu maoni ya wateja inaweza kuongeza ushindani wake kwa kuongeza ufanisi wa kampeni za uuzaji na kutoa bidhaa na huduma zinazokidhi mahitaji ya wateja. 

Mfano kama wewe ni muuzaji wa nguo basi unahitaji kuskiliza wateja wako wanapendelea nguo kutoka sehemu gani ili uweze kuwashinda wengine katika uuzaji, ushindani wa kuuza siku hizi uko katika ubora wa bidhaa na wapi unapo zitoa so jaribu sana kuchukua bidhaa zako sehemu ambayo watu wengi wanavutiwa nayo mfano Uturuki.

  • KUKUZA UAMINIFU WA WATEJA

Kusikiliza na kujibu maoni ya wateja inaweza kuimarisha uhusiano kati ya biashara na wateja wake na hivyo kukuza uaminifu wa wateja. Hata wewe ukienda katika page ya mfanyabiashara lazima utatamani akujibu ulicho muuliza ndo utaamini kama yuko serious na anacho kifanya.

Wafanyabiashara wengi wanakosea sana katika kutowajibu wateja wao bila kujua kuwa hii inakusababibisha kutoaminika kwa wateja, mfano utakuta page ya mtu inavitu vizuri unamuuliza anakwambia njo DM au nipigie kwa namber hio, hii inakuwa usumbufu kwa mteja wako kuna time mtu hana salio au hajiskii kukutafta Dm, so kama kunauwezekano anacho kuuliza mjibie hapo hapo kwenye comment kutakujengea kuaminika kwa wateja wako wote.

  • KUPATA UFAHAMU WA SOKO

Maoni ya wateja yanaweza kusaidia biashara kupata ufahamu wa kina wa soko na kuchambua mahitaji na mwenendo wa wateja. Soku zote waswahili wanasema usikasirike kukosolewa japo kuna mengine yanakera.

Hapa nikiwa na maana kuwa kuna baadhi ya maoni ya watu yatakupa ufahamu katika soko lako so usione kama amejipendekeza kukushauri jambo hilo ukamjibu vibaya, hapana jitahidi kuchukua kile unachokiona bora kutoka kwa wateja wako huwenda ndicho kitakacho kuwa chachu ya wewe kufanikiwa katika biashara yako.

Oooooh! Yaani mada ya week hii bwana tumeamua iwe fupi ili kila mtu aweze kuelewa maana jambo hili watu wengi wanaliwekea mzaha kwa kuwajibu wateja wao vibaya, mtu akikuuliza jitahidi kutumia lugha nzuri kumjibu na kumuelewa kwa wakati huo usikurupuke tuu kwa kumjibu vibaya. Kwa hivyo, ni muhimu sana kwa biashara kuzingatia maoni ya wateja na kuyatumia maoni hayo kuendeleza na kuboresha bidhaa na huduma zako.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags