Na Nnko Prisca
Lishe bora kwa mtoto ni jambo la muhimu sana na la kuzingatia sababu ndio humfanya mtoto akue katika afya nzuri ya kimwili pamoja na akili pia.
Mtoto mdogo ni tofauti kabisa na mtu mzima ambae yeye huitaji kula mara tatu kwa siku, lakini hata akirudia rudia vyakula vya aina moja haina madhara sana kama kwa mtoto.
Mtoto mdogo huitaji lishe iliyokuwa bora ili aweze kukua vizuri na awe na afya njema. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya mtoto anatakiwa kunyonya kwa muda usiopungua kwa miaka miwili ili aweze kukua vizuri.
Kuna faida kubwa sana kwa mzazi kuweza kumnyonyesha mtoto wake kwa miaka hiyo miwili, kwa mujibu wa shirika la umoja wa mataifa la mwaka 2018, wamesema kuwa mtoto anaponyonyeshwa miaka miwili mfulululizo bila kupatiwa kimiminika chochote ataepusha gharama kubwa zinazotumika kutibu magonjwa kama vile kuhara, magonjwa ya maji yasiyo safi na salama katika kumwandalia maziwa mbadala badala ya yale maziwa ya mama yake.
Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF, Henriette Fore anasema maziwa ya mama ni muhimu kwa afya ya muda mrefu ya mtoto na hupunguza gharama za matibabu ya afya kwani huepusha magonjwa kama vile kuhara. Hata hivyo suala la kumnyonyesha mtoto kwa miaka miwili mfululizo unahitaji ushirikiano kutoka ngazi ya familia hadi kitaifa.
Anasema kwa bahati mbaya hivi sasa watoto wengi wamekuwa hawapati virutubisho bora vinavyotokana na maziwa ya wazazi wao kwasababu kina mama wengi wamekuwa hawanyonyeshi watoto wao kama inavyotakiwa.
“Kuna wazazi wengine hawawanyonyeshi kabisa bali huwanunuliwa maziwa ya dukani na kuna wengine huwanyonyesha kwa muda mchache tu. Kuna utofauti mkubwa sana kati ya mtoto alienyonyeshwa na mzazi wake kwa miaka yote miwili na yule ambae amenyonya chini ya muda huo aua ambae hakunyonya kabisa.
“Kumekuwa na sababu mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwafanya kina mama kushindwa kuwanyonyesha watoto wao huku asilimia kubwa wakisema ni majukumu ya kikazi amabayo yamewabana kwa kiasi kikubwa,” anasema
Mariam Juma mama wa watoto wa tatu kutoka mikocheni yeye anasema watoto wake wote hawakufikisha miaka miwili sababu ya majukumu mengi ya kikazi hivyo alilazimika kuwanyonyesha kwa muda miezi sita na kuanzia hapo akaanza kuwapa maziwa ya dukani.
Sababu nyingine ni kifo cha mama wakati wa kujifungua. Hii imekuwa changamoto nyingine pia ambayo kwa kiasi kikubwa imepelekea watoto kukosa kunyonya maziwa ya mama yao na kupata maziwa dukani hali ambayo hufanya wapatwe na magonjwa mbalimbali sababu maziwa ya mama huwa yana kinga dhidi ya magonjwa nyemelezi kwa mtoto.
Kwa mujibu wa daktari wa wanawake katika Hospitali ya wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza, Boniface Messanga amesema maziwa yanayotoka siku ya kwanza baada ya mama kujifungua husaidia utumbo wa mtoto mchanga kukua baada ya kuzaliwa.
Anasema pia maziwa hayo husaidia kusafisha tumbo la mtoto kwa kutoa choo cha kwanza cha rangi ya kijani na kumkinga na tatizo la manjano.
Messanga anasema kuna athari kadhaa ambazo mtoto huzipata kama atakosa maziwa kutoka kwa mama yake.
“Kwa mtoto ambae labda ikatokea akakosa kabisa maziwa ya mama pale anapozaliwa anaweza akafariki au kuwa na utapia mlo wa utotoni,” anasema
Anasema utapiamlo ni changamoto ambao imekuwa ikiwapata watoto wengi ambao mara nyingi wamekosa lishe bora na hiyo sio tu kwa kukosa maziwa ya mama lakini wakati mwingine hata wale waliomaliza kunyonya vyakula ambavyo hupewa na wazazi wao husababisha utapiamlo.
Anafafanua kwa kusema siku zote chakula anachokula mtoto ni tofauti na ambacho anachokula mtu mzima hivyo ni muhimu kuzingatia mtoto anakula nini ili awe na afya bora ya mwili na kaiakili pia.
Hata hivyo anasema japo imekuwa ni changamoto sana kwa wazazi kumpatia mtoto anaeanza kula chakula ambacho ni shahihi kwake.
Kwa kawaida mtoto kuanzia umri wa miezi sita kupewa uji maalumu kama kianzio cha kuanza kula. Mara nyingi uji huo huwa mchanganyiko wa nafaka na mara nyingine mbogamboga.
Kumekuwa na unga ambao huuzwa madukani ukiwa na mchanganyiko wa nafaka tofuati tofauti kama vile mahindi, karanga, mchele, ulezi, na nafaka nyingine. Unga huu unatumika na wazazi wengi kama ndio lishe bora kwa mtoto.
Wazazi wengi wamekuwa wakiamini unga huu lakini wataalamu wamekuwa wakihoji juu ya viwango vinavyotumika katika mchanganyiko wa unga huo ambapo huatarisha usalama wake.
Amina Muhando ni mwandaaji na muuzaji wa unga lishe kwa ajili ya uji wa watoto. Yeye anasema hutumia zaidi mahindi lishe, viazi lishe na soya.
Anasema uandaaji wa unga huu unahitaji uzoefu na ufahamu mzuri wa lishe ya watoto bila kuwa makini unaweza hatarisha afya ya mtoto.
Hivyo ni muhimu kwa wazazi kujua ni kwa namna gani uji wa mtoto huandaliwa na kuepeuka kuchanganya mchanganyiko wa nafaka nyingi ambao unaweza kuleta madhara kwa mtoto. Mtaalamu wa lishe daktari louiza Tumaini Shem, anasema uji wa lishe ulio salama kwa mtoto ni ule ambao hauja wekwa vitu vingi na umechanganywa kila nafaka kwa kipimo sahihi bila kuzidisha wala kupunguza.
Aidha ameonya kama isipofanyika hivyo kunaweza tokea madhara makubwa yanayoweza kutokana na kushindwa kuandaa vyema uji wa mtoto.
Pia nafaka ambazo hazikukauka vizuri kama karanga, mahindi au yoyote ikivunda kuna sumu ambayo inaitwa inapatikana humo inaweza pia leta tatizo la ini. Hivyo ni muhimu wazazi kuwa makini kwa unga wa lishe wanaowapatia watoto wao.
Leave a Reply