Ummy Mwalimu: Wagonja hawapati huduma kisa semina

Ummy Mwalimu: Wagonja hawapati huduma kisa semina

Hivi karibuni kumekuwa na msongamano wa wagonjwa katika vituo vya Afya hali inayo pelekea baadhi ya wagonjwa kukosa huduma kwa sababau ya semina za wauguzi.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka wataalamu wa Afya nchini kupunguza semina ili kuwa na muda zaidi wa kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Julai 10, 2023 katika ziara yake Mkoani Simiyu wakati akiongea na viongozi wa mkoa huo chini ya mkuu wa mkoa Dkt. Yahaya Nawanda.

“Wataalamu wa Afya punguzeni semina maana mmekuwa na semina nyingi hadi kupelekea Wagonjwa kukosa huduma kwa wakati na kumekuwa na msomgamano mkubwa katika vituo vya kutolea huduma za afya sababu ya semina” alisema waziri huyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags