Ujumbe wa Diddy kwa mashabiki

Ujumbe wa Diddy kwa mashabiki

Mkali wa Hip-hop kutoka nchini Marekani, Diddy Combs, ame-share ujumbe kwa mashabiki uliyokuwa ukieleza kuwa muda ndio utaongea ukweli wote.

Diddy ame-share ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram uliyokuwa ukieleza kuwa “time tells truth” ukiwa na maana kuwa muda utasema ukweli, ambapo kupitia posti hiyo upande wa komenti baadhi ya mashabiki wamekuwa wakitoa maneno machafu huku wengine wakikubaliana na yeye.

Combs amekuwa akiandamwa na kesi za unyanyasaji wa kingono tangu mwaka jana 2023, huku kati ya waliowahi kumtuhumu ni aliyekuwa mpenzi wake Cassie, ambapo mpaka kufikia sasa wanasheria wake wanaendelea kupambana mahakamani na kesi hizo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post