Ujue msingi wa Mahusiano

Ujue msingi wa Mahusiano

Na Sylvia Sostenes, Msaikolojia

Mahusiano ya kimapenzi ni muunganiko wa hisia baina ya watu wawili, ambao hujengeka kuwa tabia moja, na hii inaweza kuchukua muda mrefu kujenga uhusiano ama muda mfupi kuhalalisha uhusiano.

Kisaikolojia inashauriwa kuwa mahusiano mazuri ya kimapenzi huanza na uhusiano wa kirafiki baina ya wahusika ambapo kuna mambo kadhaa wa kadhaa wahusika watajifunza ikiwemo kuzoeana, kufahamiana, kujuana kihisia.

Mfano hisia ya furaha, huzuni, hasira, wivu, hii hurahisisha kujua nama mtu flani anaweza kuridhishwa na penzi la mtu flani, ikiwa atakosewa ataombwa vipi msamaha, na inamchukua muda gani kusamehe.

Lakini pia inakupa kujua nini kinamfurahisha na nini kinamkwaza, ni nini kinamaanisha penzi kwake je! Ni outing, surprise, ama uwepo wa mtu karibu yake? Lakini nikumbushe tukuwa mahusiano yakianza na urafiki kuna manufaa makubwa mno ikiwemo kuepuka maisha ya kuigiza yaani unamjua mtu halisia na kama unaridhishwa nae unaweza ukaaanga safari ya mapenzi moja kwa moja pasipo kujipa muda wa kufanya uchunguzi.

Tukiangazia misingi ya mahusiano nitakupitisha kwenye mambo matatu ya muhimu yanayoweza kukusaidia katika safari ya mahusiano yako:-

  1. Jipende:

Kitendo cha kujipenda ni jambo kubwa na lamsingi sana linaloweza kukuimarisha kihisia kwasababu hii itakupa kujiamini na kuwavutia watu wa ngazi fulani kukuelewa na kutamani kuwa na wewe.

Si tu kuwavutia wao lakini kama utaweza kujipenda kwanza wewe maana yake utakuwa na uwezo mkubwa pia wa kumpenda mwingine. Ni jambo rahisi mno kumdhuru mwingine kama wewe mwenyewe unaweza kujidhuru. Na hautakuwa tayari kutokumpenda atakayekupenda kwasababu utahitaji ufanane nae.

  1. Jiheshimu

Mahusiano mengi yanayumba kwasababu ya heshima “heshima huja kwa anayeistahiri na si kwa anayeihitaji” watu wengi wamekuwa wakitafuta kuheshimiwa ilihali hawastahiri kuheshimiwa, heshima katika mahusiano itakufata ikiwa utatimiza maagano kati yako na mpenzi wako na heshima hii inakwenda sambamba na kutunza siri ya mahusiano yako, uwezo wa mpenzi wako kihisia, kiuchumi pia. Lakini zaidi heshimu madhaifu yako na madhaifu ya mwenzi wako maana madhaifu ndicho kipimo cha kwanza cha mapenzi.

  1. Wajibu :-

Katika mahusiano kuna watu wa aina nyingi kuna ambao hujishuguhulisha kama wazazi (parental kind of relationship or dominators) na kuna ambao watahitaji kufanyiwa tu.

Hivyo ijulikane kuwa kila mtu anawajibu wake kwenye mahusiano, kama utapenda mwenzi wako asimame kama mama basi hakikisha unasimama kama baba, na kama utataka mwenzi wako asimame kama Slay Queen basi hakikisha unasimama kama Sugar Dad kwa sababu mapenzi yapo sambamba (love goes in return).

 

  1. Msimamo

Kitu pekee kinachoweza kukuyumbisha ni msimamo hata kama utakuwa na shida kiasi gani hakikisha unakuwa na msimamo wako katika mahusiano kama ni hapana basi maanisha na kama ni ndio basi maanisha,  suala la msimamo limeweza kuyumbisha wengi  hasa kwenye kuanzisha mahusiano.

Jitahidi kutofautisha kati ya hisia, mihemko, shida na ujue namna ya kupambana na haya mambo. Katika kuanzisha mahusiano Malengo ndio kitu cha wanza kisha Hisia zitafuata nyuma.

 

  1. Ukweli

Mahusiano yananyodumu yanasimamishwa na hiki kipengere, kama ukiwa mkweli maumivu ya mapenzi yanaweza yasikundame sana kwasababu hautapoteza muda kujipa imano pasipo na ukweli.

Kama unampenda mtu mwambie kweli na kama umemkinahi mwambie pia ukweli, kwa kufanya hivyo utakuwa umeokoa muda na kujipa nafasi ya kuweza kufanya mambo mengine. Usijidanganye kwasababu uongo hutokea nyakati ambapo ukweli unajulikana. “lies are the sweetest promises “

Ustawi wa mahusiano

Usitawi wa mahusiano hutagemea vitu vikubwa vitatu, mbapo kama wawili wataanza mahusiano wakiwa wanaelewa ama kushabihiana katika haya basi watakuwa na safari nzuri na ya manufaa sana. Katika kuanzisha mahusiano yako hakikisha kuna haya mambo matatu.

Common goals (lengo yenu yawe ya kufanana ama kushabihiana) Malengo haya yanaweza yasifanane ama kushabihiana lakini basi kuwe na uwezekano wa kupata muda wa kujihusisha na malengo ya mwenzako na kuyaelewa.

Hii likifanyika hapatakuwepo na malalamiko ya kuwa busy ama kutingwa na shughuli flani ukamsahau mpenzi wako, pia utakuwa na uwezo mkubwa wa kutambua nini mpenzi wako anapitia kwenye swala la malengo.

Common interest ( kuwa na vipaumbele vinavyofanana) Hii pia itakupa kufurahia aina ya mahusisno yako kwa mfano kama wote mnapenda safari mtasafiri pamoja, kama mnapenda mziki mtaimba na kusikiliza pamoja, kama unapenda biashara basi mtakuwa pamoja. Na hii ni kwasababu mzizi wa neno mahusisno ni kuhusiana ama kuendana.

Common problems (matatizo yanayoelekeana) Kuna baadhi ya matatizo yanaweza kukuweka pamoja na haya matatizo sio lazima yawe physical problems zinaweza kuwa weakness udhaifu wa kibinadam, kwa mfano kama hupendi utani basi anayekustahiri ni mtu asiyependa utani.

Na kuna wakati unaweza kupatwa na tatizo ila mtu wako akawa wa kwanza kulibeba tatizo lako na kulitafutia ufumbuzi, na pengine kukuvumilia hadi utakapopata suluhu ya tatizo hilo.

Uimara wa mahusiano zaidi unajengwa na kuimarishwa na hayo niliyoyaeleza hapo ia cha muhimu zaidi ni kuweka mipaka ya mahusiano na kufanya jambo kwa wakati.

Kumbuka utakavyoanza ndivyo utakavyomaliza, usiingie kwenye mahusiano kama akili yako haiku sawa, hapa naaanisha utimamu wa akili unahusika kwa asilimia yoto ni lazima afya ya akili yako iwe timamu kabisa na usiwe na tatizo lolote, mfano sio kwasababu ya upweke ulio nao, sio kwasababu huna pesa, huna kazi, umechoka kufua, hapana ingia kwenye mahusiano ukiwa timamu ili usiwe mzigo kwa mwenzi wako.

NB: Kuna waliojipanga kwenda kupendwa kwenye mahusiano. Iko hivi mahusiano yanafaa sana kama utaenda kwaajili ya kupenda maana hautakaa uumizwe hasa ukikutana na mtu aliyetayari kupenda pia kwasababu mtakuwa mnapendana.

Karibu uendelee kunyoosha Hisia zako kwaajili ya mahusiano safi, makala ijayo tutaangazia wakati sahihi wa kuingia kwenye mahusiano ni upi?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags