Uhusika wa Nathan kwenye The Boys ni uhalisia wa maisha yake

Uhusika wa Nathan kwenye The Boys ni uhalisia wa maisha yake

Katika ulimwengu wa filamu, wahusika hujulikana zaidi kwa uwezo wao wa kuigiza, lakini wakati mwingine, ukweli wa maisha yao hujitokeza kwenye filamu hizo au wengine hupatiwa uhusika unaofanana na tabia zao.

Hivyo ndivyo ilivyotokea kwa mwigizaji Nathan Mitchell, anayejulikana kama Black Noir katika Filamu ya "The Boys" Season 4 ambayo aliigiza kama mtu mwenye matatizo ya kusinzia 'narcolepsy' lakini katika uhalisia inaelezwa kuwa kweli mwigizaji huyo ana tatizo hilo.

Hayo yamefichuliwa hivi karibuni na waigizaji wenzake Antony Starr na Chace Crawford walipokuwa kwenye mahojiano ya moja kwa moja na 'Podcast ya Happy Sad Confused' na kudai kuwa mkali huyo ana tatizo la kusinzia kama alivyocheza kwenye filamu.

Fahamu kuwa 'Narcolepsy' ni tatizo linalosababisha mtu kulala bila mpangilio, hata katika mazingira yasiyofaa. Kama alivyocheza Black Noir, hata hivyo katika mahojiano hayo Antony Starr na Chace Crawford walieleza walivyoweza kuingiza tatizo katika uhalisia wa muhusika na jinsi lilivyoweza kusaidia kuunda scene ambazo zinaacha kumbukumbu kwa watazamaji.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags