Uganda, Mali zasaini makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi

Uganda, Mali zasaini makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi

Uganda na Mali zimekubaliana kushirikiana kwenye mafunzo ya majeshi, ukusanyaji wa taarifa za kijasusi, operesheni za anga na ardhini pamoja na mapambano dhidi ya waasi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotangazwa na jeshi la Uganda hapo jana, Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Vincent Ssempijja na mwenzake wa Mali, Kanali Sadio Camara, walisaini makubaliano hayo mjini Kampala.

Ssempijja alisema Uganda ina hamu ya kuingia kwenye ushirikiano wa kiulinzi kwa imani ya udugu wa Kiafrika na kuimarisha usalama wa bara hilo. Kanali Kamara kwa upande wake alisema Mali itafaidika na utaalamu wa jeshi la Uganda.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post