Ufaransa vijana kupewa condom bure

Ufaransa vijana kupewa condom bure

Inasemekana kuwa Kuanzia Mwezi huu wa January,2023 Vijana wa Ufaransa wataagana rasmi na bajeti za kununua condom kwakuwa condom zitaanza kugaiwa bure kwenye maduka yote nchini humo.

Taasisi mbalimbali na mitaani hii ikiwa ni hatua muhimu inayolenga kupunguza magonjwa ya zinaa kama ukimwi, Kaswende na Kisonono pamoja na kupunguza mimba zisizotarajiwa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza hatua hizo za kiafya akisema Vijana watakuwa huru kujipatia condom bure hadi kwenye maduka ya dawa ambapo Serikali itabeba mzigo wa kulipia condom hizo, hatua hiyo imepewa jina la “Mapinduzi madogo ya kujikinga”

Aidha mwaka 2020 na 2021 Ufaransa ilishuhudia 30% ya ongezo la magonjwa ya zinaa ambapo Rais Macron amesema Ufaransa ilikuwa na changamoto ya elimu kwenye elimu ya uzazi.

Hii itawahusu Vijana kuanzia miaka 18 badi 25 ambapo lengo ni kuwasaidia pia kupunguza mimba zisizotarajiwa kwakuwa Vijana wenye umri huo wengine hawana uwezo wa kumudu gharama za kutumia uzazi wa mpango.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags