Ubinafsi katika biashara

Ubinafsi katika biashara

Mambo zenu guyz I hope mko powa kabisa, sasa kama kawaida yetu mwenzo ni ule ule katika segment yetu ya biashara, ni kupeana madeal tuu kuhusiana na ujasiriamali.

Bwana kuna kitu hapa najua wengi wenu mtaungana na mimi kuhusiana na swala zima la ubinafsi, hapa naomba tulizungumze kwa ujumla kwanza, ubinafsi ni tabia ya mtu kujipendelea mwenyewe na kutojali wengine na je kitu hichi katika biashara kinaweza kukubalika ungana nasi mwanzo mpaka mwisho kufahamu Zaidi kuhusu hili…

Na leo tutabase sana katika ubinafsi wa kutokuwa na huruma na wale walio izunguka biashara yako hii ni moja ya sababu inayo sababisha biashara nyingi zinazo anzishwa kupotea ndani ya muda mfupi.

Biashara zilizo anzishwa na kufanikiwa kusimama kwa muda mrefu mara nyingi waanzilishi wa biashara hizo huweka kipaumbele kwa makundi muhimu manne na kuhakikisha yameridhika na huduma itolewayo..
Makundi haya manne ni:
✓ Wateja,
✓ Wafanyakazi / Team
✓ Wenye hisa zao kwenye biashara na,
✓ Washirika wa biashara.

Takwimu inaonyesha biashara za makampuni makubwa ulimwenguni zina hakikisha makundi haya manne ya watu yameridhika na kuweka misingi bora ya
✓ Furaha Kazini,
✓ Uaminifu,
✓ Ukweli,

✓ Uwazi,
✓ uwajibikaji,

Kabla ya Kuanzisha biashara jichunguze kama upo tayari kulipa gharama za kuhakikisha makundi hayo manne ya watu wanao izunguka biashara yako hayana changamoto ya kukosa:-
✓ Uaminifu wako,
✓ upendo wako,
✓ ukweli na uwazi.

Endapo ukijua una mapungufu ya kutanguliza maslahi yako mwenyewe katika kila jambo kwenye biashara unayotaka kuianzisha basi ni muhimu kuwa na mtaalamu wa kukuongoza, mwenye ujuzi na uwezo wa kusimamia rasilimali katika kuleta matokeo katika biashara hii itakusaidia kuepusha athari za biashara kudondoka.

Nimeeleza kwa uchache sana na natumai kuwa tumeelewa, kuna baadhi ya wafanyabiashara wanaleta ubinafsi wa nyumbani na mitaani kwao mpaka katika biashara, hii kitu haipendezi kabisa biashara ni jambo amablo umelichagua wewe mwenyewe kwa ajili ya kuwatumikia watu so achana na mambo hayo ya kibinafsi.

Unachotakiwa kukijua ni kuepuka ubinafsi na kujiangalia mwenyewe katika safari yako ya kuanzisha biashara, kumbuka unajitoa kwa ajili ya jamii na inabidi ufanye jambo kwa ajili ya jamii, mifano ipo mingi sana kama akina Vunjabei, Bakhresa wamejitoa na kufanya biashara kwa ajili ya jamii wewe usiangalie utaingiza faida bei gani.

Nasemajeee nasemajeeee!!! Yaani wafanyabiashara wote tuko kwa ajili ya wateja wetu na sio manufaa yetu. Usiache kutembelea mitandao yetu ya kijamii @Mwananchiscoop kwaajili ya kujifunza mambo mbali mbali kuhusiana na biashara, burudani, michezo na fashion.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post